Fabio Da Silva anataka kuondoka Manchester United baada ya kusema ameshindwa vita kupata namba katika kikosi cha kwanza ndano ya Old Trafford.
Ingawa kaka yake Rafael amekuwa katika kikosi cha kwanza cha United katika nafasi ya ulinzi wa kulia Fabio anakuwa nyuma ya walinzi wengine wa kushoto Patrice Evra na Alex Buttner .
Read more............
Pengine lingekuwa ni anguko kubwa kabisa kwake endapo David Moyes angefanikiwa kuwanasa Leighton Baines au nyota wa Real Madrid Fabio Coentrao wakati wa uhamisho wa majira ya kiangazi
Fabio mwenye umri wa miaka 23 alitumia msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya QPR na ameitumikia United mchezo mmoja katika kampeni ya mwaka huu.
Alikuwa ni miongoni mwa wachezaji watatu wa kikosi cha kwanza wakiwemo akina Ashley Young na Buttner, katika mchezo wa kirafiki uliochezwa bila ya watazamaji dhidi ya Barnsley siku ya Jumatatu.
Fabio, ambaye aliwasili pamoja na ndugu yake Old Trafford wakitokea katika klabu ya Fluminense mwaka 2008, amemuambia Moyes kuwa anapendea kuondoka mwezi Januari na angependelea kurejea nchini Brazil.
CHICHARITO ATAJA SABABU KWA NINI ATAONDOKA MAN UNITED
Anaangalia mbele: Javier Hernandez akiwa mazoezini na kikosi cha timu yake ya taifa ya Mexico wiki hii
Mshambuliaji huyo anayefahamika kama Chicharito hapewi nafasi kubwa katika klabu ingawa mwezi uliopita aliifungia timu hiyo bao la ushindi katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One dhidi ya Liverpool na zaidi ya mechi hiyo alianza katika mechi nyingine moja tu, United ikifungwa nyumbani na West Brom.
Hernandez amesema kwamba wakati akiwa ana furaha kuchezea klabu kubwa kama hiyo, pia anataka nafasi zaidi za kucheza na anaamini anaweza kuwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza iwe Old Trafford au katika klabu yoyote.
Alichemsha: Hernandez hakuweza kufunga katika mechi yake nyingine pekee aliyoanza msimu huu dhidi ya West Brom
"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.
"Nafanyia kazi hilo- kupata nafasi kikosi cha kwanza. Nafahamu kwamba kiwango changu uwanjani kitaniruhusu kutimiza lengo hilo siku fulani, aidha hapa [Manchester] au popote katika klabu yoyote.
"Naelekea kutimiza miaka minne hapa [Manchester United] na kweli, kama ambavyo wakati wote nimesema, nina furaha kuwa tayari nimechezea moja ya klabu bora duniani, nafanya vizuri kila siku kutafuta muda zaidi uwanjani,".

Shujaa: Chicharito alifunga bao la ushindi United ikiwafunga wapinzani wake wa jadi, Liverpool Uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita
"Nahitaji kupewa nafasi zaidi kuonyesha uwezo wangu, kwa sababu kati yetu sote tunataka kutoa mchango wetu ili hii timu ishinde ubingwa,".
Hernandez amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza United kutokana na kuzidiwa kete na akina Wayne Rooney, Robin van Persie na Danny Welbeck, lakini Mmexico huyo amesema hiyo inaweza kuwa nzuri kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu England.
"Ushindani ndani ya timu wakati wote umekuwa mkubwa na ninafikiri hiyo inaisaidia timu kwa kiasi kikubwa, kwa sababu kuna wachezaji wengi bora ambao kila mmoja kati yao anataka nafasi kikosi cha kwanza,".
"Mazoezi na mechi zinazokuja zitatulazimisha kusimama imara kuisaidia timu kuimarika kwa vyote, kwa uchezaji binafsi na kitimu kwa ujumla,".
Hivi Moyes anaweza kuwa 'chizi' kumruhusu Hernandez kuondoka? Hizi ni takwimu za washambuliaji wa United katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa, ambazo zinaonyesha ni mshambuliaji mkali zaidi United...

No comments:
Post a Comment