Social Icons

Saturday, 12 October 2013

VAN PERSIE AVUNJA REKODI YA MABAO YA KLUIVERT UHOLANZI AKIFUNGA HAT TRICK USIKU HUU

Kiwango cha dunia: Robin van Persie sasa ni mfungaji bora wa kihistoria Uholanzi
MSHAMBULIAJI Robin van Persie amekuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi kufutaia kufunga mabao matatu peke yake (hat trick) usiku huu katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Hungary.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United aliingia katika mchezo huo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, akiwa ana mabao 38 katika mechi 78 za Orange, na wenyeji hawakuwa na presha kwa kuwa walikwishajihakikishia tiketi ya Brazil Septemba mwakani.

Read more......
Van Persie alifunga dakika ya 16 kabla ya Kevin Strootman na Jeremain Lens kuongeza.
Nahodha wa The Orange akafikia rekodi ya mabao 40 ya Patrick Kluivert karibu na mapumziko na akashangilia kwa kumkumbatia Kluivert, ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa Louis van Gaal katika timu hiyo.
Van Persie akavunja rekodi hiyo kwa bao la dakika ya 53 baada ya kazi nzuri ya Arjen Robben -- ambaye pia alimpa van Persie pasi ya bao la pili kabla ya kumpisha Dirk Kuyt dakika ya 61, Uholanzi wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 8-1.
Mabao mengine ya Uholanzi yamefungwa na Strootman dakika ya 25, Jens dakika ya 38, Devecseri akajifunga dakika ya 65, Van der Vaart dakika ya 86 na Robben dakika ya 90, wakati la Hungary lilifungwa na Dzsudzsak kwa penalti dakika ya 47.

Ameondolewa kileleni: Patrick Kluivert ndiye alikuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi

No comments:

Post a Comment