Social Icons

Thursday, 10 October 2013

Kama ulikuwa hufahamu,Fahamu sasa wachezaji watano kutoka Afrika watakaocheza ligi ya NBA 2013/2014



Carlos Morais amesajiliwa kuichezea TORONTO RAPTORS msimu huu akiwa na uzoefu wa kuiongoza Angola kwenye mashindano kadhaa ya kimataifa na amewahi kucheza kwenye mashindano ya FIBA Afrika 2005 na 2007, mashindano ya dunia mwaka 2006 pamoja na mashindano ya Olimpiki mwaka 2008.

Ripoti hii imeandaliwa na dstv.com
  
Read more.......
 Hasheem Thabeet (Tanzania)

Ndio mchezaji mrefu kuliko wote kwenye ligi ya NBA kwa sasa, majuzi wakati timu yake ya Oklahoma City Thunder ikicheza na Charlotte Bobcats Hasheem alicheza vunds 10, huu utakua msimu wake wa pili akiwa na OKC. 


Gorgui Dieng (Senegal)

Dieng (23) amesajiliwa na Minnesota Timberwolves baada ya kufanya vizuri akiwa na timu ya Louisville Cardinals inayoshiriki ligi ya vyuo vikuu Marekani NCAA.
Ike Diogu (Nigeria)

Ike ni mchezaji wa kiafrika ambae amewahi kucheza ligi ya NBA kwa muda mfupi kabla ya kwenda barani Asia alikochezea timu ya XINJIANG FLYING TIGERS, GUANGDONG SOUTHERN TIGERS na timu mbili za PUERTO RICO ambazo ni CAPITANES DE ARECIBO na LEONES DE PONCE ila kwa sasa anarejea kwa mara ya pili kwenye ligi ya NBA ambapo atachezea timu ya NEW YORK KNICKS.
Bismack Biyombo (DRC)

Unaambiwa moja ya majina makubwa kwenye mchakato wa kuchagua wachezaji wanaotoka vyuoni mwaka 2011 lilikua jina la Bismack Biyombo ambae alichaguliwa na timu ya SACRAMENTO KINGS na mwaka huu amesajiliwa na CHARLOTTE BOBCATS ambako atakua akishindana kutafuta namba na Cody Zeller aliyejiunga na timu hiyo msimu huu..


No comments:

Post a Comment