

Wanajeshi wa Kenya wakati waliopokuwa wakizingira Kituo cha Biashara cha Westgate kilichoshambuliwa na magaidi
Miili miwili iliyoungua vibaya
aliyoopolewa katika eneo la kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya
siku ya Alhamisi inawezekana kwa kiasi kikubwa ikiwa ni ya magaidi
walioshambulia kituo hicho, Mbunge mmoja wa Kenya ameiambia BBC.
Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati ya Bunge
inayochunguza shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao
umepatikana unawezekana kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa
wanajeshi.