Atletical madrid Leo wametwaa Taji la Ubingwa wa Spain kwa mara ya kwanza baada
ya Miaka 18 baada ya kutoka Sare ya Bao 1-1 na Barcelona waliokuwa
wakicheza kwao Uwanjani Nou Camp.
Barcelona ndio walitangulia kufunga
katika Dakika ya 32 kwa Bao la Alexis Sanchez na Atletico kusawazisha
Dakika ya 49 kwa Bao la Diego Godin.Kwenye Mechi hii, Atletico walimpoteza Mfungaji wao Bora, Diego Costa, ambae alilazimika kutoka baada kuumia.Atletico wamemaliza La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Barcelona na Real Madrid.FA CUP: UKAME MIAKA 9 WAISHA, ARSENAL WATWAA KOMBE!
BAADA
kukaa Miaka 9 bila Kombe lolote, baada kutwaa FA CUP Mwaka 2005, Leo
hii Uwanjani Wembley, Jijini London, Arsenal wamefanikiwa kubeba FA CUP
walipotoka nyuma kwa Bao 2-0 ndani ya Dakika 8 za kwanza na kushinda 3-2
katika Dakika 120 za Gemu.Hadi Dakika 90, Bao zilikuwa 2-2 na
Dakika za Nyongeza 30 zikaongezwa na Aaron Ramsey kuifungia Arsenal Bao
la ushindi katika Dakika ya 109.Hull City walitangulia kwa kuongoza Bao 2-1 katika Dakika 8 za kwanza tu na Arsenal kupata Bao la Kwanza Dakika ya 17.Arsenal walisawazisha kwenye Dakika ya 71 na Gemu kumalizika 2-2 katika 90 za Mchezo na ndipo zikaja Dakika za Nyongeza 30.
Tazama jinsi arsenal walivyoshangilia ubingwa hapa
FAINALI 2014 DFB-Pokal: BAYERN WATWAA KOMBE BAADA DAKIKA 120!
BAO
za Arjen Robben na Thomas Muller ndani ya Kipindi cha Pili cha Dakika
za Nyongeza 30, baada Mechi kumalizika 0-0, zimewapa Bayen Munich Kombe
la Ujerumani, 2014 DFB-Pokal, kwa kuifunga Borussia Dortmund Bao 2-0
kwenye Fainali iliyochezwa Olympiastadion huko Berlin.Kwenye Mechi hii inayokutanisha Vigogo
wa Germany ambao walimaliza Bundesliga kwa Bayern kuwa Bingwa na
Dortmund kushika Nafasi ya Pili, na inayobatizwa'Der Klassiker',
Dortmund walifunga Bao Safi katika Kipindi cha Pili baada Frikiki ya
Nuri Sahin kuunganishwa kwa Kichwa na Mats Hummels na Mpira kuonekana
kuvuka Mstari wa Golini lakini Refa hakutoa Bao hilo.Hadi Dakika 90, Bao zilikuwa 0-0 na
zikaja Dakika za Nyongeza 30 na Bayern kufunga Bao zao Dakika ya 107
kupitia Robben na Dakika ya 120 kwa Bao la Muller,
Tazama hapa jinsi Beyern walivyo wafanya mbaya Borusia Dortimund
No comments:
Post a Comment