Social Icons

Saturday 10 May 2014

Wakenya wang'ara Diamond League


Bingwa mara mbili wa dunia mkenya Asbel Kiprop na mkenya mwenzake Hellen Obiri walianza msimu wa mashindano ya Diamond League mjini Doha Qatar kwa kishindo baada ya kushinda mbio zao mtawalia Ijumaa usiku.Kiprop alimaliza wa kwanza katika mbio za mita 1,500 kwa dakika 3 sekunde 29.
Mwenzake waliyekimbia naye Silas Kiplagat alimaliza wa pili kwa dakika tatu sekunde 33.Kwa upande wa wanawake, Obiri, alivunja rekodi ya Afrika ya mbio za mita 3000 baada ya kuzimaliza kwa dakika 8:20.68.Mkenya mwenzake Mercy Cherono alikuwa wa pili na dakika nane sekunde 21.Wakenya hao wawili wamekuwa wakimbiaji waliomaliza mbio hizo kwa kasi zaidi kuliko katika mashindano mengine yoyote ya Diamond League.Muethiopia Genzebe Dibaba alimaliza wa sita.

No comments:

Post a Comment