Tanzania, ikicheza Nyumbani Jijini Dar
es Salaam, Leo imeifunga Zimbabwe Bao 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya
Raundi ya Pili ya Mtoano ya AFCON 2015 kuwania kucheza Fainali huko
Morocco Mwaka 2015.
Katika Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Bao pekee na la ushindi kwa Taifa Stars lilifungwa na Straika wa Azam FC, John Bocco, katika Dakika ya 15 baada kuunganisha Krosi ya Thomas Ulimwengu anaecheza TP Mazembe ya Congo DR.Timu hizi zitarudiana huko Harare Wikiendi ya kuanzia Mei 30 na Mshindi atacheza na Mshindi kati ya Mozambique na South Sudan kwenye Raundi inayofuata ambayo ndio itatoa Timu moja kuingia KUNDI F kujumuika na Zambia, Niger na Cape Verde.

VIKOSI:
TAIFA STARS: Deo
Munishi, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin
Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Mbwana
Samatta, Thomas Ulimwengu.
ZIMBABWE: George Chigova, Partson Jaure, Danny
Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen Alimenda, Rendai Ndoro, Milton Ncube,
Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila, Peter Moyo, Eric Chipeta.
REFA: Joseph Odartei Lamptey [Ghana]
REFA: Joseph Odartei Lamptey [Ghana]
No comments:
Post a Comment