Watu wengi huko Uingereza hii
ni nafasi murua kwa Arsene Wenger na Arsenal yake kumaliza ukame wao wa
Miaka 9 bila ya Kombe lolote wakati Jumamosi watakapoingia Wembley
Stadium Jijini London kuivaa Hull City kwenye Fainali ya FA CUP.
Arsenal wanapambana na Hull City ambao
wamemaliza Msimu huu wakiwa Nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu England lakini
kwa Meneja wa Hull City, Steve Bruce, Nguli wa Man United, faraja kubwa
ni kukumbuka nini kiliwakuta Arsenal Miaka mitatu iliyopita walipotinga
Wembley kwenye Fainali ya Kombe la Ligi na kuchapwa 2-1, bila
kutarajiwa, na Birmingham City.Wakiwa na Masupastaa kama kina Mesut
Ozil, Santi Cazorla na Olivier Giroud, utabiri wote unanyoosha kidole
kuwa Arsenal ndio Bingwa wa FA CUP na hasa ukizingatia Rekodi mbovu ya
Hull City dhidi ya Arsenal ya kufungwa Mechi zote 2 za Ligi Kuu England
Msimu huu na pia kutoifunga Arsenal tangu wakutane uso kwa uso kuanzia
Mwaka 2009.
SAFARI KWENDA WEMBLEY
ARSENAL Raundi ya 3 Arsenal 2 Tottenham 0 Raundi ya 4 Arsenal 4 Coventry 0 Raundi ya 5 Arsenal 2 Liverpool 1 Raundi ya 6 Jumamosi Machi 8 Arsenal 4 Everton 1 Nusu Fainali Wigan 1 Arsenal 1 [Penati: Arsenal 4-2] |
HULL CITY Raundi ya 3 Middlesbrough 0 Hull City 2 Raundi ya 4 Southend 0 Hull City 2 Raundi ya 5 Brighton 1 Hull City 1 [Marudiano Hull 2 Brighton 1] Raundi ya 6 Hull City 3 Sunderland 0 Nusu Fainali Hull City 5 Sheffield United 3 |
Wenger anatarajiwa kufanya uamuzi nani
amuweke Golini kati ya Kipa Lukas Fabianski, ambae amedaka Mechi zao
zote za FA CUP Msimu huu, au Kipa Nambari Wani Wojciech Szczesny, ambae
ametwaa Glovu za Dhahabu Msimu huu baada ya kuweka Rekodi ya kutofungwa
katika Mechi 16 za Ligi Kuu England.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Arsenal: Fabianski; Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Ramsey, Arteta; Ozil, Cazorla, Podolski; Giroud
HULL CITY: Harper; Bruce, Chester, Davies, Figueroa, Rosenior; Livermore, Huddlestone, Elmohamady; Boyd; Sagbo
REFA: Lee Probert
No comments:
Post a Comment