David Luiz hii Leo alikuwa Jijini Paris
akikamilisha taratibu zake za kuhamia Paris Saint-Germain na akiwa huko
alitoa salaam za shukrani kwa Klabu yake Chelsea ambako kuna taarifa
Mmiliki wa Klabu hiyo Roman Abramovich ametoa idhini kuwa Dau la kumuuza
Mbrazil huyo apewe Jose Mourinho kununua Wachezaji wapya.
Huko Paris, Luiz amekuwa akipimwa Afya
yake na kukamilisha Mazungumzo ya maafikiano ya malupulupu yake binafsi
taratibu ambazo zinategemewa kukamilika hii Leo.David Luiz ameuzwa kwa PSG kwa Dau la
Pauni Milioni 50 zikimfanya awe ndie Beki wa Bei ghali Duniani na Fedha
zote hizo zitakwenda kwa Jose Mourinho kununua Wachezaji wapya huku
Straika wa Atletico Madrid, Diego Costa, ambae Mkataba wake una
Kipengele cha kulipwa Dau la Pauni Milioni 31.5 ikiwa atauzwa wakati
Mkataba wake haujaisha, akitajwa kuwa ni mmoja wa walengwa wakuu wa
Mourinho.
Vilevile zipo taarifa zinamuhusisha Mourinho na Viungo Paul Pogba wa Juventus na Paulinho wa Tottenham.Zipo kila dalili kuwa Mourinho anahaha kumpata Staa mkubwa kabla Fainali za Kombe la Dunia kuanza huko Brazil hapo Juni 12.
Akiongea na Jarida 'Globo Esporte.',
David Luiz alituma ujumbe wa shukran ambapo alisema: “Asante Chelsea kwa
Miaka 3 ½ ya uhusiano mzuri. Nimepata Marafiki, Mechi na Mataji ambayo
daima yataishi kwenye fikra zangu! Nawashukuru Wafanyakazi, Wachezaji na
Mashabiki”Luiz aliichezea Chelsea Mechi 143 tangu ahamie hapo kutoka Benfica ya Ureno.
No comments:
Post a Comment