Straika wa Manchester United Javier
Hernandez ‘Chicharito’ ametajwa miongoni mwa Wachezaji 23 wa Timu ya
Taifa ya Mexico ambayo itacheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil
kuanzia Juni 12.Licha ya kutokuwa na namba ya kudumu
kwenye Klabu yake Man United ambako ameanza Mechi 6 tu za Ligi Kuu
England Msimu huu,
Chicharito yumo kwenye Timu ya Kombe la Dunia ambako
huko Brazil wamepangwa Kundi A pamoja na Wenyeji Brazil, Cameroun na
Croatia.Mexico wamefuzu kucheza huko Brazil kwa kupitia Mechi za Mchujo walipoitoa New Zealand.Mchezaji maarufu wa Mexico ambae ameachwa ni Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela, ambae sasa yuko Real Sociedad.Mexico watacheza Mechi ya Kwanza ya
Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil hapo Juni 13 dhidi ya Cameroun na
kisha kuzivaa Brazil na Croatia.Kila Nchi inayocheza Fainali inatakiwa
ipeleke Majina ya Wachezaji wao wasiozidi 30 kwa FIFA ifikapo Mei 13 na
Listi ya mwisho ya Wachezaji 23 inatakiwa iwasilishwe Juni 2.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Jesus Corona (Cruz Azul), Guillermo Ochoa (Ajaccio), Alfredo Talavera (Toluca)
MABEKI: Rafael Marquez
(Leon), Diego Reyes (Porto), Hector Moreno (Espanyol), Paul Aguilar
(America), Miguel Layun (America), Carlos Salcido (Tigres), Francisco
Maza Rodriguez (America), Miguel Layun (América), Andres Guardado (Bayer
Leverkusen)
VIUNGO: Jose Juan
Vazquez (Leon), Juan Carlos Medina (America), Hector Herrera (Porto),
Carlos Pena (Leon), Luis Montes (Leon), Marco Fabian (Cruz Azul), Isaac
Brizuela (Toluca)
MAFOWADI: Oribe Peralta
(Santos Laguna), Javier Hernandez (Manchester United), Raul Jimenez
(America), Alan Pulido (Tigres), Giovani dos Santos (Villarreal)
No comments:
Post a Comment