Social Icons

Sunday 25 May 2014

Mbwana Samata ainusuru Tp Mazembe Cuf Champion Ligi


Mbwana Samata Straika mahiri wa Tanzania, Jioni hii huko Stade TP Mazembe, Lubumbashi, Congo DR, alifunga Bao pekee katika Dakika ya 62 wakati Tmu yake TP Mazembe ilipoitungua AS Vita Club, pia ya Congo DR, Bao 1-0 katika Mechi ya KUNDI A la CAF CHAMPIONZ LIGI.
Hizi ni Mechi za Pili kwa kila Timu katika Kundi lao na katika Mechi ya Kwanza, TP Mazembe ilifungwa Bao 1-0 na Al Hilal huko Sudan na AS Vita Club kuichapa Al Zamalek ya Misri Bao 2-1 walipocheza Mjini Kinshasa.

Hapo Jana, kwenye Mechi nyingine ya KUNDI A, Al Zamalek iliichapa A l Hilal ya Sudan Bao 2-1.TP Mazembe na AS Vita Club ni Timu zenye upinzani mkali mno Nchini Congo DR ambao ulipelekea Watu 15 kufa Uwanjani walipokutana huko Kinshasa Wiki kadhaa nyuma wakati Mazembe ikishinda Bao 1-0 kwenye Mechi ya Ligi.

No comments:

Post a Comment