Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi Uingereza "kufanya kile itakachoweza" kusaidia kuwapata wasichana wa shule zaidi ya 200 waliotekwa na magaidi wa Boko Haram.Bwana Cameron amesema hayo wakati alipopokea karatasi ya iliyosainiwa kauli mbiu"#Bring Back Our Girls" yaani warejeshe wasichana wetu,
wakati wa kipindi cha BBC cha Andrew Marr.
Bwana Cameron ni kiongozi wa hivi karibuni wa juu kuunga mkono kampeni ya vyombo vya habari vya mitandao ya kijamii baada ya mke wa rais wa Marekani Michelle Obama alipopigwa picha kiwa na karatasi yenye maandishi kama hayo.Wapiganaji wa Kiislam wa kikundi cha Boko Haram wamedai kuhusika na utekaji wa wasichana hao.Wakati wa programu hiyo ya BBC, mgeni mwaalikwa Christiane Amanpour, mwandishi wa habari mkuu wa kimataifa wa CNN, alimkabidhi bwana Cameron karatasi lenye maandishi ya "#Bring Back Our Girls" na kumwuliza kama angependa kujiunga na kampeni hiyo.
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama akiwa katika kampeni ya kutaka kurejeshwa kwa wasichana waliotekwa Nigeria.Akichukua karatasi hiyo,
"Pia, hebu tu wakweli, hapa Uingereza bado kuna vikundi vyenye kuunga mkono misimamo mikali ya kidini,ambayo tunatakiwa kukabiliana nayo, iwe mashuleni, vyuoni au vyuo vikuu na kwingineko.."
Anaelewa kuwa si kazi rahisi kuwatafuta wasichana, ambao walitekwa kutoka shuleni kwao Chibok tarehe 14 Mei 2014 katika jombo la Borno.Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis pia naye ametuma ujumbe wa tweeter akiunga mkono kampeni ya kurejeshwa wasichana hao akiandika: "tuungane katika maombi ili kuachiliwa haraka kwa wanafunzi hao wa kike waliotekwa nchini. #BringBackOurGirls."
No comments:
Post a Comment