Social Icons

Monday 12 May 2014

Boko Haram Waonyesha wasichana waliotekwa

Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.

Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyoRais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

No comments:

Post a Comment