Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limesikitishwa
na hatua ya kutekwa nyara kwa zaidi ya wasichana 200 wa shule nchini
Nigeria na kundi la wanamgambo wa kiislamu la boko haram.Baraza hilo pia limeshtumu mashambulizi ya hivi
karibuni ya kundi hilo,huku likitaka wale wanaotekeleza vitendo kama
hivyo kukamatwa mbali na kuwekewa vikwazoWataalam wa Marekani,
Uingereza na Ufaransa wamewasili nchini Nigeria ili kusaidia kuwatafuta wasichana hao.Marekani na Uingereza zinasema kuwa zitalipatia kipaumbele ombi la Nigeria la kutuma ndege za upelelezi.Wakati huohuo Katika tukio ambalo si la kawaida,
mke wa rais wa Marekani Michelle Obama anatarajiwa kutoa taarifa ya
kila juma ya mumewe itakayoangazia utekaji nyara wa wasichana wa shule
nchini Nigeria.Wake wa marais kwa kawaida hukataa kujihusisha
na sera za kigeni ,lakini bi. Obama amekuwa mkosoaji mkubwa wa kundi la
wanamagambo wa kiislamu ambao waliwateka nyara wasichana hao.Awali bi Obama aliweka picha katika mtandao wa tweeter ilio na maneno yanayosema 'Warudisheni wasichana wetu'.
Saturday 10 May 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment