Mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya
Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itafanyika Jumapili
(Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Awali mechi hiyo tulipanga ichezwe
Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa yote ya
Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
Ili Uwanja wa Sokoine uweze kuchezwa
mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo Jumamosi (Mei
10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika
hayatamalizika katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.Tunatoa mwito kwa wamiliki wote wa
viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze maboresho ya
kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango
vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA).Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
Monday 12 May 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment