Social Icons

Saturday 24 May 2014

Bobby Zamora Airejesha QPR Ligi kuu England Apiga Goli Dakika 90 Tazama Hapa


Bao la dakika ya 90 la Bobby Zamora limewarudisha Queens Park Rangers LIGI KUU ENGLAND Msimu ujao baada ya kuifunga Derby County Bao 1-0 kwenye Fainali ya Mechi za Mchujo za Daraja la Championship
huku wakicheza pungufu kwa zaidi ya Dakika 30 za mwisho baada ya Kadi Nyekundu kwa Beki wao Gary O'Neil.QPR sasa wanaungana na Leicester City na Burnley kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao.Leicester City na Burnley, kwa kumaliza Nafasi za 1 na 2 kwenye Daraja la Championship, zilifuzu kucheza moja kwa moja Ligi Kuu England.QPR na Derby zilifuzu kucheza Fainali hii baada ya kuzibwaga Wigan na Brighton kwenye Mechi za Awali zilizochezwa Nyumbani na Ugenini mapema Mwezi huu.Mechi hizi za Mchujo zilihusisha Timu za Daraja la Championship zilizomaliza Nafasi za 3 hadi za 6 kwani Timu mbili za Juu ndio pekee hupanda Ligi Kuu England moja kwa moja.Kwenye Fainali ya Leo, hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.Kuanzia Dakika ya 60, QPR walilazimika kucheza Mtu 10 baada ya Beki wao Gary O'Neil kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Refa Lee Mason baada kumchezea Rafu Straika wa Derby Russell.

          QPR wakishangilia kombe kupanda ligi kuu England

Kuanzia hapo, Derby walitawala na kukosa nafasi kadhaa na pia kukwamishwa na Sentahafu Richard Dunne wa QPR na Kipa wake Robert Green waliosimama imepanda Ndipo likaja Goli Dakika ya 90 ambalo lilifungwa na Straika Bobby Zamora alieingizwa Kipindi cha Pili.Bao hilo lilianzia kwa Mpira wa kurushwa na Hoilett akapeleka Krosi ya chini Golini na Beki Keogh kuokoa fyongo na kumpelekea Mpira Zamora ambae hakujivunga na alipiga Mpira wa Juu uliomshinda Kipa Grant.Sasa QPR, na Meneja wao maarufu Harry Redknapp, wamerudi tena Ligi Kuu England baada ya kushushwa Daraja Msimu mmoja tu uliopita Mwezi Mei Mwaka Jana. 

Tazama hapa jinsi Bobby Zamora Alivyofunga goli
 
VIKOSI:
Derby: Grant, Wisdom, Keogh, Buxton, Forsyth, Hendrick, Thorne, Hughes, Russell, Martin, Ward
Akiba: Bryson, Eustace, Sammon, Legzdins, Whitbread, Dawkins, Bamford.

QPR: Green, Simpson, Onuoha, Dunne, Hill, Doyle, Barton, O'Neil, Hoilett, Austin, Kranjcar
Akiba: Traore, Morrison, Yun, Hughes, Henry, Zamora, Murphy.
Refa: Lee Mason (Lancashire)

MATOKEO:
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumapili Mei 11
Derby County 4 Brighton and Hove Albion 1 [6-2]
Jumatatu Mei 12.
Queens Park Rangers 2 Wigan Athletic 1 [2-1]
Jumamosi Mei 24
[Saa za Bongo]
Fainali - Wembley Stadium
Derby County 0 QPR 1

No comments:

Post a Comment