Sunday 11 May 2014
Mkataba wa usitishaji uhasama nchini Sudan kusini umeanza kutekelezwa
Mkataba wa usitishaji uhasama kati ya serikali ya rais Salva kiir na waasi wanaoongozwa na Riek Machar nchini Sudan kusini umeanza kutekelezwa mda mfupi uliopita .Msemaji wa rais Salva Kiir ameiambia BBC kwamba vikosi vya serikali vina haki ya kulipiza kisasi iwapo waasi watakiuka mkataba huo na basi kuvishambulia.
Hatahivyo msemaji huyo Ateny Wek Ateny amesema kuwa serikali ya Sudan Kusini haina mpango wa kuzua vita vyovyote.Amekana kwamba vita hivyo vya miezi mitano vilibadilika na kuwa vya kikabila kati ya kabila la Dinka na Lile la Nuer.Vita hivyo vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku zaidi ya wengine millioni moja wakiwachwa bila makao.Awali Umoja wa mataifa ulizitaka pande zote mbili kusaidia katika kuhakikisha kuwa misaada ya dharura inawafikia waathiriwa wa vita hivyo kufuatia kutiwa sahihi kwa makubaliano hayo.
Labels:
AddyTz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment