Leo, kuanzia Saa 1 Usiku,FC Barcelona wanaingia Uwanjani kwao Nou Camp kucheza na Atletico Madrid
wakijua ushindi kwenye Mechi hii ya mwisho ya La Liga utawapa Ubingwa
wao wa 5 huko Spain katika Miaka 6.
Lakini, Atletico Madrid, ambao ndio
Vinara wa La Liga kwa Pointi 3 mbele ya Barcelona, wanataka Sare tu ili
watwae Ubingwa kwa mara ya kwanza tangu 1996.Kwenye Mechi yao ya Leo, Barca itamkosa
Mchezaji wao wa Siku nyingi, Carles Puyol, ambae alikwisha kutangaza
kustaafu Soka mwishoni mwa Msimu huu kutokana na kukabiliwa na tatizo la
Goti kwa muda mrefu.Puyol, Miaka 36, alianza kuichezea Barca tangu Oktoba 1999.Mbali ya Puyol, Barca inatarajiwa
kuwakaribisha tena Majeruhi wao waliokuwa nje hivi karibuni aMbao ni
Neymar,alekuwa nje Mwezi, Gerard Pique na Jordi Alba.Atletico Madrid watakuwa nae Straika wao hatari Diego Costa ambae amekuwa akisumbuliwa na Musuli za Pajani [Hamstring].
Mahesabu ya Mechi ya Leo:
-USHINDI kwa Barcelona: BINGWA Barcelona
-SARE: BINGWA Atletico
-USHINDI kwa Atletico: BINGWA Atletico
Akiongelea kutocheza Mechi hii ambayo
ndio ingekuwa yake ya kuaga kabla kustaafu, Puyol amesema: “Nimezungumza
na Makocha na kwa sababu hii ndio itaamua Bingwa ni bora wakacheza wale
waliokuwa fiti Asilimia 100!”Ikiwa hii Leo Barca watashinda basi
watafungana kwa Pointi na Atlwtico Madrid na Barca watapewa Ubingwa kwa
kuwa na Matokeo Bora ya Uso kwa Uso kati yao kwa vile Timu hizi zilitoka
0-0 katika Mechi ya Kwanza huko Vicente Calderon.
Ni mara mbili tu katika Historia ya La
Liga Bingwa amepatikana baada Timu mbili kufungana kwa Pointi na Ubingwa
kuamuliwa kwa kutazama Matokeo ya Uso kwa Uso kati ya Timu hizo mbili.Hali hii ya Bingwa kupatikana kwa
Matokeo ya Uso kwa Uso ilitokea Msimu wa 1950/51 wakati Atletico
walipowapiku Sevilla na mara nyingine ilikuwa ni Miaka 5 kabla ya hapo.
Uso kwa Uso 2013-14:
21 Agosti: Atletico 1-1 Barcelona (Spanish Super Cup)
28 Agosti: Barcelona 0-0 Atletico (Spanish Super Cup)
11 Januari: Atletico 0-0 Barcelona (La Liga)
1 Aprili: Barcelona 1-1 Atletico (UEFA CHAMPIONS LIGI)
9 Aprili: Atletico 1-0 Barcelona (UEFA CHAMPIONS LIGI)
Ikiwa Atletico watwaa Ubingwa, hii
itakuwa ni mara yao ya kwanza katika Miaka 18 na wataondoa himaya ya
Real Madrid na Barcelona kubadilishana Ubingwa ambayo imedumu kuanzia
Mwaka 2004 Valencia walipotwaa Ubingwa.Akizungumzia Mechi hii, Kocha wa
Atletico, Diego Simeone amesema: “Wachezaji wamefanya kazi kubwa sana.
Kutufikisha nafasi hii, Siku ya mwisho ya Msimu, tukishindana na Timu
Bora kutwaa Ubingwa ni kitu ambacho ngumu kukirudia. Wamefika hapa kwa
kustahili!”
LA LIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Atletico de Madrid |
37 |
28 |
5 |
4 |
76 |
25 |
51 |
89 |
2 |
FC Barcelona |
37 |
27 |
5 |
5 |
99 |
32 |
67 |
86 |
3 |
Real Madrid CF |
37 |
26 |
6 |
5 |
101 |
37 |
64 |
84 |
4 |
Athletic de Bilbao |
37 |
20 |
9 |
8 |
66 |
39 |
27 |
69 |
Kwa La Liga, ikiwa Timu zinafungana kwa Pointi, ili kuamua nani yuko Juu, Matokeo ya Uso kwa Uso kati ya Timu hizo mbili ndio huamua nani Bora na SIO MAGOLI!!
**Ikiwa Matokeo ya Uso kwa Uso yanalingana, Magoli ndio hufuatwa!!
LA LIGA
Mechi za mwisho
Ijumaa Mei 16
Malaga CF 1 Levante 0
[Saa za Bongo]
Jumamosii Mei 17
1700 Real Madrid CF v RCD Espanyol
1900 FC Barcelona v Atletico de Madrid
2300 Valencia v Celta de Vigo
Jumapili Mei 18
1300 Real Sociedad v Villarreal CF
1900 Osasuna v Real Betis
1900 Rayo Vallecano v Getafe CF
1900 Real Valladolid v Granada CF
1900 UD Almeria v Athletic de Bilbao
2200 Sevilla FC v Elche CF
No comments:
Post a Comment