Social Icons

Friday, 9 May 2014

Francis Miyeyusho kesho kwenye ukumbi wa PTA ulingoni na MATUMLA

Francis Miyeyusho kesho kwenye ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam atajaribu kurejesha heshima wakati atakapopigana na Mohamed Matumla katika pambano lisilo la ubingwa, uzito wa Feather baada ya Aprili 19, mwaka huu kupigwa vibaya na Sukkassem Kietyongyuth wa Thailand.
Lakini kuna wasiwasi pambano la kesho likawa chungu tena Miyeyusho ‘Chichi Mawe’, kwani ni takriban wiki tatu tangu apigwe Mthailand na hakuna hakika kama alipata muda mzuri wa kupumzika na kujiandaa na pambano lingine.

Ikumbukwe Miyeyusho alipigwa na Sukkassem kwa Knockout (KO) raundi ya kwanza sekunde ya 55 katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa, uzito wa Feather lililofanyika ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam.Katika pambano hilo lililohudhuriwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova aliyekuwa mgeni rasmi, Miyeyusho aligoma kupanda ulingoni kwa dakika zaidi ya 20 akishinikiza kwanza alipwe fedha zake.Kamanda Kova ambaye mdogo wake, Mussa Kova ndiye aliyeandaa mapambano hayo kupitia kampuni yake ya Mawenzi Production, aliingilia sakata hilo na bondia huyo akalipwa fedha zake akapanda ulingoni.Dalili za Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ kupigwa zilionekana wakati nyimbo za taifa zinapigwa, kwani alikuwa asiyejiamini na mwenye kihoro, hivyo kumpa nafasi Mthailand kulianza kwa kasi pambano hilo

No comments:

Post a Comment