Social Icons

Tuesday 20 May 2014

Luis Enrique Meneja mpya Barcelona kwa Mkataba wa Miaka wa miwili


Barcelona jana imemteua Luis Enrique kama Meneja wao mpya kwa Mkataba wa Miaka wa miwili.Luis Enrique, Miaka 44, anambadili Gerardo Martino ambae Juzi alitangaza kuachia ngazi baada ya kushindwa kuisaidia Barca kutetea Taji lao la La Liga.
Ijumaa, Enrique alijiuzulu kama Meneja wa Celta Vigo akiwa katikati ya Mkataba wake wa Miaka miwili.Hii ni mara ya tatu kwa Enrique kuwa pamoja na Barcelona ambako Mwaka 1996 alijiunga kama Mchezaji akitokea Real Madrid na kuichezea Klabu hiyo mara zaidi ya 200 na kustaafu Mwaka 2004.Mwaka 2008, Enrique alishika wadhifa wa Kocha wa Barcelona B na kuiwezesha kupanda Daraja kuingia Daraja la Pili katika Mwaka wa Pili.Wakati huo huo, Barcelona imethibitisha kumasaini Kipa wa Klabu ya Borussia Mönchengladbach ya Germany, Marc-Andre Ter Stegen, na pia kuwarudisha kutoka kwenye Mikopo Wachezaji wao wawili, Gerard Deulofeu, aliekuwa Everton ya England na Rafa Alcântara aliekuwa Celta Vigo ya Spain.

No comments:

Post a Comment