Gerardo Martino ataacha kazi ya Ukocha
wa Barcelona mara baada ya Jana kupokonywa Ubingwa wa La Liga baada
kutoka Sare 1-1 na Atletico Madrid ambao wameutwaa Ubingwa huo na
kuiacha Barca ikitoka mikono mitupu Masimu huu kitu ambacho hakijawahi
kutokea tangu 2007/08.
Akizungumza mara baada ya Mechi hiyo ya
Jana, Martino alisema: “Nasikitika sana tumeshindwa kutimiza malengo
yetu ambayo Klabu hii Siku zote imeyaweka na kutimiza!”Martino alishika wadhifa huo Mwezi Julai Mwaka Jana na kumbadili Tito Vilanova ambae alijiuzulu baada kuugua.Kazi yake hapo Barcelona ilikuwa ya
kwanza kwa Martino, Raia wa Argentina, nje ya Marekani ya Kusini tangu
ashike wadifa wa Ukocha wa Miezi 6 huko Tenerife, Spain.
Akiwa na Barca, Martino alisimamia
ushindi wa Mechi 40 kati ya 59 lakini wakapokonywa Ubingwa wa La Liga,
kutupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenye Robo Fainali na kufungwa
Fainali ya Copa del Rey na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment