Social Icons

Sunday 11 May 2014

Mourinho amesema anaamini Edin Dzeko, na sio Luis Suarez,ndie anastahili Tuzo ya Mchezaji Bora


MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amesema anaamini Edin Dzeko, na sio Luis Suarez,ndie anastahili kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa LIGI KUU ENGLAND.Suarez ndie alietwaa Tuzo za Mchezaji Bora za PFA [Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa] na FWA [Chama cha Waandishi Habar wa Soka] kwa Msimu huu.
Mara nyingi Mourinho amekuwa akimponda Suarez na ameshawahi kumbatiza kuwa ni ‘Mfalme wa Penati’ na pia ‘Mcheza Sarakasi wa Bwawa la Kuogelea’ kwa kujirusha kwake ili kuhadaa Marefa apate Penati.Mourinho amedai hata Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, alistahili Tuzo hiyo na si Suarez.Mourinho amesema: “Suarez ni Mchezaji mzuri. Hawampigii Kura Mchezaji ambae si Bora. Lakini Mchezaji Bora ni lazima awe na sifa na tabia nzuri kama walivyokuwa wakiteua Miaka 10, 8, 6 iliyopita!”
Hapo alikumbushia jinsi Suarez alivyomng’ata Meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic Msimu uliopita na kufungiwa Mechi 10 ingawa aligusia hilo si tukio la Msimu huu.Aliongeza: “Mchezaji Bora anatoka kwa Mabingwa! Kama Bingwa ni Man City, wanahitaji Pointi 1, basi ningemchagua Edin Dzeko!”Mourinho amesema: “Dzeko si Mfungaji tu. Anasaidia, Anacheza, Ametulia, Ana haki na wala hatafuti Wachezaji kuadhibiwa kwa kujirusha! Hakuwa na namba pale City lakini alipochaguliwa alileta tofauti kubwa! Kwa sasa ana Bao 16 na Bao 16 kwa Straika wa Tatu kwenye Timu ni kitu cha ajabu!”Kuhusu Gerrard, Mourinho alimsifia na kusema ni Mpigaji Penati mzuri sana lakini pia anaisaidia Timu yake kushinda.

No comments:

Post a Comment