NCHI 32 ambazo zitacheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil kuanzia Juni 12 zipo mbioni kutangaza na kuwasilisha Vikosi vyao vya Awali vya Wachezaji wasiozidi 30 kwa FIFA kabla ya Siku ya mwisho hapo Mei 13.Listi za mwisho za Wachezaji 23 kwa Timu hizo 32 zinapaswa kutua FIFA ifikapo Juni 2.
LEO HII RUSSIA, ALGERIA na GHANA, zimetangaza Vikosi vyao.Awali Leo, Japan na England zilitaja Wachezaji wao.
RUSSIA YATAJA TIMU YA BRAZIL, PAVLYUCHENKO NJE!
MASTAA wa Klabu ya Lokomotiv Moscow,
Roman Pavlyuchenko na Dmitry Tarasov, wameachwa kwenye Kikosi cha Russia
cha Awali cha Wachezaji 30 waliotajwa na Kocha Fabio Capello ambae pia
ameshangaza wengi kwa kumuita Straika Mkongwe Pavel Pogrebnyak, mwenye
Miaka 30, ambae anacheza Daraja la Championship huko England na Klabu ya
Reading.Russia wanatarajiwa kujipima nguvu na Slovakia hapo Mei 26, Norway Mei 31 na Morocco hapo Juni 6.Huko Brazil, Russia, ambao hii ni mara
ya kwanza kucheza Fainali za Kombe la Dunia tangu Mwaka 2002, wapo KUNDI
H pamoja na Belgium, South Korea na Algeria.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA:Igor Akinfeev (CSKA Moscow), Yury Lodygin (Zenit St Petersburg), Sergei Ryzhikov (Rubin Kazan)
MABEKI: Alexander
Anyukov (Zenit St Petersburg), Alexei Berezutsky, Vasily Berezutsky,
Sergei Ignashevich, Georgy Shchennikov (all CSKA Moscow), Vladimir
Granat, Alexei Kozlov (both Dynamo Moscow), Andrei Yeshchenko (Anzhi
Makhachkala), Dmitry Kombarov (Spartak Moscow), Andrei Semenov (Terek
Grozny)
VIUNGO: Igor Denisov,
Yury Zhirkov (both Dynamo Moscow), Alan Dzagoev (CSKA Moscow), Yury
Gazinsky, Roman Shirokov (both FC Krasnodar), Denis Glushakov (Spartak
Moscow), Pavel Mogilevets (Rubin Kazan), Viktor Faizulin, Oleg Shatov
(both Zenit St Petersburg)
MAFOWADI: Vladimir
Bystrov (Anzhi Makhachkala), Alexander Kerzhakov (Zenit St Petersburg),
Artem Dzyuba (Rostov), Alexei Ionov, Alexander Kokorin (both Dynamo
Moscow), Maxim Kanunnikov (Amkar Perm), Pavel Pogrebnyak (Reading/ENG),
Alexander Samedov (Lokomotiv Moscow)
ALGERIA YATANGAZA 30
Algeria, chini ya Kocha Vahid
Halilhodzic, imetangaza Kikosi chake cha Wachezaji 30 kwa ajili ya
Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil zinazoanza Juni 12 na wapo
Wachezaji kadhaa wanaocheza huko England.
Chipukizi wa Tottenham Nabil Bentaleb na
Kiungo wa Leicester City Riyad Mahrez, ambae ameitwa kwa mara ya
kwanza, wanaungana na Rafik Djebbour wa Nottingham Forest kwenye Timu
hiyo.Bentaleb aliingizwa Timu ya Kwanza ya
Tottenham mara baada kuteuliwa Meneja Tim Sherwood na Mwezi Machi
aliamua kuichezea Algeria kwa mara ya kwanza badala ya France
alikozaliwa.Riyad Mahrez ameitwa kwa mara ya kwanza
kuichezea Algeria na Kocha Vahid Halilhodzic amekiri kumwona Mchezaji
huyo aliezaliwa France mara ya kwanza Mwezi Februari na kuvutiwa mno.Huko Brazil , Algeria wako KUNDI H pamoja na Belgium, Russia na South Korea.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Azzedine Doukha
(USM El Harrach), Rais Mbolhi (CSKA Sofia), Cedric Si Mohamed (CS
Constantine), Mohamed Lamine Zemmamouche (USM Alger)
MABEKI: Essaid Belkalem
(Watford), Madjid Bougherra (Al Lekhwiya), Liassine Cadamuro
(Mallorca), Faouzi Ghoulam (Naples), Rafik Halliche (Academica Coimbra),
Nacereddine Khoualed (USM Alger), Aissa Mandi (Stade Reims), Carl
Medjani (Valenciennes), Djamel Mesbah (Livorno), Mehdi Mostefa (Ajaccio)
VIUNGO: Nabil Bentaleb
(Tottenham Hotspur), Ryad Boudebouz (Bastia), Yacine Brahimi (Granada),
Abdelmoumene Djabou (Club Africain), Sofiane Feghouli (Valencia), Adlene
Guedioura (Crystal Palace), Foued Kadir (Stade Rennes), Amir Karaoui
(Entente Setif), Mehdi Lacen (Getafe), Riyad Mahrez (Leicester City),
Saphir Taider (Inter Milan), Hassan Yebda (Udinese)
MAFOWADI: Rafik Djebbour (Nottingham Forest), Nabil Ghilas (Porto), Islam Slimani (Sporting), El Arabi Soudani (Dinamo Zagreb).
GHANA YATANGAZA 26!
Ghana, chini ya Kocha Akwasi Appiah,
imetaja Kikosi chake cha Awali cha Kombe la Dunia na wamo Magwiji wao
wote kina Michael Essien na Sulley Muntari wa AC Milan, Kevin
Prince-Boateng wa Schalke na Asamoah Gyan anaecheza Al Ain ya Falme za
Nchi za Kiarabu.
Ghana watacheza Mechi ya Kirafiki na Holland hapo Mei 31 na baadae kupunguza Kikosi hicho kufikia Wachezaji 23.
MAKIPA: Stephen Adams (Aduana Stars), Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset)
MABEKI: Harrison Afful
(Esperance), Jerry Akaminko (Eskisehirspor), John Boye (Stade Rennes),
Samuel Inkoom (Platanias), Jonathan Mensah (Evian Thonon Gaillard),
Daniel Opare (Standard Liege), Jeffrey Schluup (Leicester City), Rashid
Sumaila (Mamelodi Sundowns)
VIUNGO: David Accam
(Helsingborg), Afriyie Acquah (Parma), Albert Adomah (Middlesbrough),
Emmanuel Agyemang Badu (Udinese), Kwadwo Asamoah (Juventus), Christian
Atsu (Vitesse Arnhem), Andre Ayew (Olympique Marseille), Michael Essien
(AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar), Sulley Muntari (AC Milan),
Mubarak Wakaso (Rubin Kazan)
MAFOWADI: Jordan Ayew (Sochaux), Kevin Prince Boateng (Schalke 04), Asamoah Gyan (Al Ain), Abdul Majeed Waris (Valenciennes).
No comments:
Post a Comment