Milipuko miwili ilitikis Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi na kuwaua watu 10 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa.Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa.
Mlipuko wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea upande wa pili wa soko.
Soko la Gikomba ni maarufu kwa nguo za mitumba
Milipuko ya leo imetokea siku moja baada ya
Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi nchini humo kurejea makwao
kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari kutolewa ya kutokea kwa
mashambulizi ya kigaidi nchini humo.Gikombaa ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.Kenya imekuwa ikikumwba na mashambulizi ya mara
kwa mara kutoka kwa wawatu wenye uhusiano na kundi la wanamgambo la
kiisilamu nchini Somalia la Al Shabaab.
No comments:
Post a Comment