Social Icons

Saturday 10 May 2014

Ronaldo atarajia Usiku wa Kichawi Fainali Uefa Champions League


Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesema Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya Real Madrid na Atletico Madrid itakayochezwa hapo Mei 24 huko Lisbon, Ureno ipo '50-50'.Hata hivyo, Nyota huyo ambae ndie Nahodha wa Timu ya Taifa ya Porugal, amesema anatarajia Usiku huo utakuwa ‘Usiku wa Kichawi’ kwa Timu yake Real Madrid ambayo inawania kutwaa Taji lake la 10 la Ubingwa wa Ulaya walioubatiza ‘LA DECIMA’.
Hii itakuwa ni Fainali ya kwanza ya Real kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu Mwaka 2002.Pia, Ronaldo ametoboa kuwa Fainali hiyo itakuwa ngumu kuitabiri pale alipotamka: “Huu ni wakati ambao Klabu imeungoja kwa muda mrefu. Itakuwa Fainali nzuri, Mechi ya kufurahisha kwa Timu mbili Bora. Fainali Siku zote ni 50-50,. Tunaomba Usiku huo uwe mzuri kwetu na tushinde. Tunaomba Mei 24 uwe ‘Usiku wa Kichawi’ kwa Real Madrid!”Msimu huu, Real tayari wameshabeba Kombe la Copa del Rey na bado wapo kwenye kinyang’anyiro cha La Liga ingawa nafasi yao ni finyu kwani Atletico wako kileleni wakiwa Pointi 4 mbele huku Mechi zimebaki 2.

UEFA CHAMPIONZ LIGI
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014
[Saa 3 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu]
Real Madrid v Atletico Madrid
Refa: Bjorn Kuipers [Holland]

Uso kwa Uso Msimu huu:
-Real na Atletico zimekutana mara 4.
-LA LIGA: Sept 28=Atletico 1 Real 0, Machi 2=Real 2 Atletico 2
-Copa del Rey: Feb 5=Real 3 Atletico 0, Feb11=Atletico 0 Real 2

No comments:

Post a Comment