Sunday, 11 May 2014
Mapigano yazuka upya Sudan Kusini
Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wamelaumiana kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano - masaa tu baada ya makubaliano kufikiwa.
Msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, alisema wapiganaji wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu leo alfajiri.Wapiganaji wamewashutumu wanajeshi wa serikali kuwa waliwashambulia katika sehemu kadha katika majimbo ya Upper Nile na Unity.Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni moja kuhama makwao.
Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi Riek Machar wakitia sahihi mkataba wa kusitisha vita kwa masaa 24 nchini humo.
Labels:
AddyTz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment