Social Icons

Saturday 10 May 2014

EPL Msimu wa 2013-2014 Kumalizila Kesho Jumapili Cheki Tathimini fupi hapa



MSIMU wa 2013-14 wa LIGI KUU ENGLAND unafika tamati Jumapili huku kukiwa na vitu kadhaa vikiwa haviajaamuliwa ikiwa ni pamoja na Nani Bingwa.

-Manchester City kutulia na kubakisha Ubingwa Jijini Manchester?
Manchester City wanahitaji Sare tu kwenye Mechi yao ya mwisho hapo Jumapili Uwanjani kwao Etihad dhidi ya West Ham kwa vile wao wana Tofauti Bora ya Magoli, Goli 13, ukulinganisha na Timu ya Pili Liverpool ambayo inahitajika kuifunga Newcastle Uwanjani Anfield na kuomba City wafungwe ili wao watwae Ubingwa wao wa kwanza tangu Mwaka 1990.

-Man City au Liverpool kuvunja Rekodi ya kufunga Bao nyingi Msimu mmoja kwenye Ligi Kuu England?
Baada Man City kuifunga Aston Villa Bao 4-0 Jumatano iliyopita, wamefikisha Bao 100 kwa Msimu mmoja wa Ligi na Liverpool wana Bao 99 hadi sasa.Klabu hizo zinainyemelea Rekodi ya Chelsea ya kufunga Bao 103 waliyoiweka Msimu wa 2009/10 chini ya Meneja Carlo Ancelotti.

-Luis Suarez kuvunja Rekodi ya Bao nyingi Msimu mmoja?
Luis Suarez anazo Bao 31 za Ligi sawa na Rekodi ya Alan Shearer na Cristiano Ronaldo ya kufunga Bao hizo kwenye Ligi Kuu England yenye Mechi 38 za Msimu mmoja.Lakini, kwenye Ligi Kuu England, yenye Mechi 42 za Msimu mmoja, Rekodi hiyo inashikiliwa na Alan Shearer na Andy Cole ambao walifunga Bao 34 kila mmoja.


 **FAHAMU: LIGI KUU ENGLAND ilikuwa na Timu 22 ilipoanzishwa Mwaka 1992 na kupunguzwa kuwa Timu 20 Mwaka 1995 na kisha Timu 20 Mwaka 2007.

-Tottenham kuizuia Man United kucheza EUROPA LIGI?
Tottenham wanahitaji Sare tu kwenye Mechi yao ya Nyumbani na Aston Villa ili kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao lakini wakifungwa na Man United kuifunga Southampton, basi Man United ndio watakamata Nafasi ya 6 na kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao.

-Nani wanaaga Ligi Kuu England?
VIDIC_ZOEZI 












Nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic tayari ameshaaga rasmi na anakwenda kuchezea Inter Milan na Mechi ya Jumapili na Southampton ndio ya mwisho kabisa kwake lakini wenzake Ryan Giggs, Patrice Evra na Rio Ferdinand wanamaliza Mikataba yao na hadi sasa haijulikana kama watapewa nyongeza.Huko Chelsea, John Terry, Frank Lampard na Ashley Cole huenda nao wakawa wanacheza Mechi zao za mwisho kwa vile pia Mikataba yao inamalizika.Kwa upande wa Mameneja hamna uhakika kwa Meneja wa Spurs, Tim Sherwood, na mwenzake wa Aston Villa, Paul Lambert, kama watakuwepo Msimu ujao.

-Norwich kushuka?
Kwenye kushuka Daraja, tayari Timu 2, Cardiif City na Fulham, zimeshateremka tangu Wikiendi iliyopita na bado Timu moja lakini Norwich City ndio wenye uhakika mkubwa wa kuporomoka kwani kubaki kwao itakuwa miujiza mikubwa sana kwa vile, kwanza wanahitaji kushinda na pili West Bromwich Albion wafungwe lakini hayo pia hayatoshi kwani Matokeo hayo yanahitaji yaambatane na mabadiliko ya Tofauti ya Magoli kubwa sana.WBA wana Pointi 36 na Tofauti ya Magoli -15 na Norwich wana Pointi 33 na Tofauti ya Magoli -32 na hivyo kufungwa kwa WBA na kushinda kwa Norwich lazima kubadilishe Tofauti ya Magoli kwa idadi ya Goli 17. 

2013-2014 Barclays Premier League  Table
 





 
POS
TEAMPWDLFA
WDLFA
WDLFA
GDPts
1 Manchester City 37 26 5 6 100 37
16 1 1 61 13
10 4 5 39 24
63 83
2 Liverpool 37 25 6 6 99 49
15 1 2 51 17
10 5 4 48 32
50 81
3 Chelsea 37 24 7 6 69 26
15 3 1 43 11
9 4 5 26 15
43 79
4 Arsenal 37 23 7 7 66 41
13 5 1 36 11
10 2 6 30 30
25 76
5 Everton 37 20 9 8 59 39
13 3 3 38 19
7 6 5 21 20
20 69
6 Tottenham Hotspur 37 20 6 11 52 51
10 3 5 27 23
10 3 6 25 28
1 66
7 Manchester United 37 19 6 12 63 42
9 3 7 29 21
10 3 5 34 21
21 63
8 Southampton 37 15 10 12 53 45
8 5 5 31 22
7 5 7 22 23
8 55
9 Newcastle United 37 15 4 18 42 57
8 3 8 23 28
7 1 10 19 29
-15 49
10 Stoke City 37 12 11 14 43 51
10 6 3 27 17
2 5 11 16 34
-8 47
11 Crystal Palace 37 13 5 19 31 46
8 3 8 18 23
5 2 11 13 23
-15 44
12 West Ham United 37 11 7 19 40 49
7 3 9 25 26
4 4 10 15 23
-9 40
13 Swansea City 37 10 9 18 51 53
6 5 8 33 26
4 4 10 18 27
-2 39
14 Sunderland 37 10 8 19 40 57
5 3 10 20 24
5 5 9 20 33
-17 38
15 Aston Villa 37 10 8 19 39 58
6 3 10 22 29
4 5 9 17 29
-19 38
16 Hull City 37 10 7 20 38 51
7 4 7 20 19
3 3 13 18 32
-13 37
17 West Bromwich Albion 37 7 15 15 42 57
4 9 5 23 25
3 6 10 19 32
-15 36
18 Norwich City 37 8 9 20 28 60
6 6 6 17 16
2 3 14 11 44
-32 33
19 Fulham 37 9 4 24 38 83
5 2 11 22 36
4 2 13 16 47
-45 31
20 Cardiff City 37 7 9 21 31 72
5 5 8 19 33
2 4 13 12 39
-41 30

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Mechi za Mwisho za Msimu
Jumapili 11 Mei 2014
[Mechi zote Saa 1100 Jioni, Saa za Bongo]
Cardiff v Chelsea
Fulham v Crystal Palace
Hull v Everton
Liverpool v Newcastle
Man City v West Ham
Norwich v Arsenal
Southampton v Man United
Sunderland v Swansea
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Stoke

No comments:

Post a Comment