Social Icons

Sunday 11 May 2014

Manchester City Bingwa Ligi Kuu England


Manchester City Leo hii wametwaa Ubingwa wao wa Pili ndani ya Miaka mitatu baada ya kuwafunga West Ham Bao 2-0 katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanjani kwao Etihad na kuhakikisha Kombe hilo la Ubingwa wa England linabaki Jijini Manchester na pia kuikatili Liverpool
waliokuwa na ndoto kubwa za kutwaa Ubingwa wao wa kwanza tangu Mwaka 1990





MAN_CITY-MABINGWA_2014-WATU_WAVAMIA_UWANJA




Man City, waliokuwa Mabingwa wa England kwa mara ya mwisho Mwaka 1968 wakati huo ikiwa ni Daraja la Kwanza, walitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu wa 2011/12 chini ya Meneja Roberto Mancini kwa kuipiku Man United kwa Tofauti ya Magoli na Msimu uliofuatia, ule wa 2012/13, Man United waliwabwaga City na kurudisha Ubingwa huo kwa Tofauti ya Pointi 11.

GERRARD-YOU_WILL_ALWAYS_WALK_ALONE 
Safari hii, Man City, baada kusambaratika Man United kufuatia kustaafu Sir Alex Ferguson na Timu kuchukuliwa na David Moyes, walichuana vikali na Arsenal, Chelsea na hasa Liverpool ambao walisalimu amri mwishoni.Pamoja na Leo hii Man City kutwaa Ubingwa uliosababisha Mashabiki wao kuvamia Uwanja mara baada ya Mechi kwisha Uwanjani Etihad, pia Tottenham walijihakikishia kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao baada kuifunga Aston Villa Bao 3-0 na kumaliza Nafasi ya 6.Kwenye Mechi za Ulaya za UEFA Msimu ujao, England itawakilishwa na Mabingwa Man City, Liverpool, Chelsea na Arsenal kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Everton, Spurs na Hull City [kwa kutinga Fainali ya FA CUP na Arsenal ambao wako UEFA CHAMPIONZ LIGI], zitacheza EUROPA LIGI.

Manchester City-Misimu yao ya Ubingwa:
[MARA 4]
-1936-37
-1967-68
-2011-12
-2013-14

TAARIFA FUPI ZA MECHI ZOTE 10 ZA MWISHO ZA LIGI:
MANCHESTER CITY 2 WEST HAM 0
Bao za City zilifungwa na Samir Nasri, Dakika ya 39, na Vincent Kompany, Dakika ya 49.
VIKOSI
MANCHESTER CITY: Hart; Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov; Nasri, Garcia, Toure, Silva; Aguero, Dzeko
Akiba: Pantilimon, Lescott, Clichy, Milner, Fernandinho, Negredo, Jovetic.
WEST HAM: Adrian; O'Brien, Tomkins, Reid, McCartney; Taylor, Noble; Downing, Nolan, Diame; Carroll
Akiba: Jarvis, Armero, Vaz Te, Collins, Jaaskelainen, C Cole, J Cole.
Refa: Martin Atkinson.

LIVERPOOL 2 NEWCASTLE 1
Newacastle walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 20 baada Skrtel kujifunga mwenyewe na Liverpool kusawazisha kwa Bao la Agger Dakika ya 63 na Sturridge kupiga Bao la Pili Dakika ya 65.
Newcastle walimaliza Mechi hii Mtu 9 baada Shola Ameobi, Dakika ya 66, na Dummets, Dakika ya 87, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
VIKOSI:
LIVERPOOL: Mignolet; Johnson, Skrtel, Agger, Flanagan; Henderson, Gerrard, Allen; Sterling, Suarez, Sturridge
Akiba: Jones, Toure, Sakho, Cissokho, Lucas, Coutinho, Aspas.
NEWCASTLE: Krul; S.Taylor, Williamson, Coloccini, Haidara; Debuchy, Anita, Tiote, Gouffran; Sissoko; Shola Ameobi
Akiba: Elliot, Santon, Yanga-Mbiwa, Satka, Dummett, Sammy Ameobi, de Jong.
Refa: Phil Dowd

SOUTHAMPTON 1 MAN UNITED 1
Southampton walitangulia kufunga kwa Bao la Rickie Lambert, aliempiga kipepsi Nemanja Vidic, lakini Man United walisawazisha kwa frikiki safi ya Juan Mata.
VIKOSI:
SOUTHAMPTON: Boruc, Clyne, Fonte, Lovren, Shaw, Wanyama, Cork, Schneiderlin, Davis, Lallana, Lambert.
Akiba: Ward-Prowse, Do Prado, Chambers, Gazzaniga, Hooiveld, Reed, Gallagher.
MANCHESTER UNITED: De Gea; Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra; Januzaj, Fletcher, Kagawa, Welbeck; Mata; van Persie.
Akiba: Hernandez, Carrick, Young, Cleverley, Valencia, Lawrence, Amos.
Refa: Mike Dean

NORWICH CITY 0 ARSENAL 2
Bao za Kipindi cha Pili za Ramsey na Jenkinson zimewapa ushindi Arsenal.
VIKOSI:
NORWICH: Ruddy; Martin (c), R Bennett, Turner, Olsson; Tettey; Snodgrass, Howson, Johnson, Redmond; Elmander.
Akiba: Whittaker, Fer, Hooper, Bunn, Elliott Bennett, Loza, Murphy.
ARSENAL: Fabianski, Jenkinson, Sagna, Koscielny, Gibbs, Arteta, Rosicky, Ramsey, Ozil, Podolski, Giroud
Akiba: Szczesny, Wilshere, Monreal, Flamini, Sanogo, Diaby, Kallstrom.
Refa: Lee Mason
SUNDERLAND 1 SWANSEA CITY 3
MAGOLI:
-Sunderland: Dakika ya 50 Borini
-Swansea: Dakika ya 7 Dyer, 14 Emnes na 54 Bony.
VIKOSI:
SUNDERLAND: Mannone, Vergini, Bardsley, Brown, O'Shea (c), Bridcutt, Larsson, Colback, Johnson, Borini, Wickham
Akiba: Celustka, Altidore, Ba, Giaccherini, Mavrias, Agnew, Ustari.
SWANSEA CITY: Tremmel, Tiendalli, Amat, Bartley, Taylor (C), Fulton, Shelvey, Dyer, Emnes, Routledge, Bony
Akiba: Cornell, Williams, Davies, Britton, de Guzman, King, Vazquez.
Refa: Chris Foy

CARDIFF CITY 1 CHELSEA 2
Cardiff walitangulia kufunga Dakika ya 15 kupitia Mkongwe Craig Bellamy na Chelsea kupigia Bao zao Dakika ya 73 kupitia Andre Schurrle na Dakika ya 76 kwa Bao la Fernando Torres.
VIKOSI:
CARDIFF CITY: Marshall, Fabio, Caulker, Turner, John, Gunnarsson, Mutch, Whittingham, Daehli, Bellamy, Campbell.
CHELSEA: Schwarzer, Ivanovic, Cole, Azpilicueta, Kalas, Oscar, Mikel, Salah, Hazard, Matic, Torres.
Refa: Michael Oliver

FULHAM 2 CRYSTAL PALACE 2
MAGOLI:
-Fulham: Amorebieta, Dakika ya 58, na David, Dakika ya 90
-Palace: Gayle, Dakika ya 28 84
VIKOSI:
FULHAM: Stockdale, Zverotic, Heitinga, Hangeland, Amorebieta, Kacaniklic, Sidwell, Parker, Richardson, Rodallega, Woodrow
Akiba: Kasami, Mitroglou, Dejagah, David, Joronen, Williams, Tunnicliffe.
CRYSTAL PALACE: Hennessey, Mariappa, Dann, Delaney, Ward, Bolasie, Jedinak, Ledley, Ince, Chamakh, Gayle
Akiba: Speroni, Dikgacoi, O'Keefe, Puncheon, Murray, Gabbidon, Jerome.
Refa: Kevin Friend

TOTTENHAM 3 ASTON VILLA 0
Bao za Spurs zilipachikwa na Paulinho, Baker, kwa kujifunga mwenyewe na Penati ya Adebayor.
VIKOSI:
SPURS: Lloris, Naughton, Dawson, Chiriches, Rose, Sigurdsson, Sandro, Paulinho, Eriksen, Adebayor, Kane
Akiba: Soldado, Capoue, Friedel, Fryers, Pritchard, Bentaleb, Veljkovic.
ASTON VILLA: Guzan, Lowton, Baker, Vlaar, Bertrand, Westwood, Bacuna, Delph, Weimann, Bowery, Agbonlahor
Akiba: Clark, El Ahmadi, Steer, Sylla, Holt, Robinson, Grealish.
Refa: Jon Moss

HULL CITY 0 EVERTON 2
Bao za Everton zilifungwa na McCarthy na Lukaku.
VIKOSI:
HULL: McGregor, McShane, Bruce, Davies, Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Quinn, Figueroa, Aluko, Jelavic
Akiba: Rosenior, Koren, Fryatt, Boyd, Sagbo, Long, Harper.
EVERTON: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McGeady, McCarthy, Barry, Osman, Naismith, Lukaku
Akiba: Robles, Hibbert, Deulofeu, Pienaar, Traore, Alcaraz, McAleny.
Refa: Howard Webb 

WEST BROM 1 STOKE 2
West Ham walifunga Bao lao katika Dakika ya 56 kupitia Sessegnon na Stoke kupata Bao Dakika ya 22 kwa Mc Auley kujifunga mwenyewe na Bao la ushindi kufungwa na Adam Dakika ya 87.
VIKOSI:
WEST BROM: Foster, Dawson, McAuley, Olsson, Brunt, Morrison, Mulumbu, Dorrans, Amalfitano, Sessegnon, Berahino
Akiba: Yacob, Ridgewell, Myhill, Lugano, Anichebe, Vydra, O'Neil.
STOKE: Sorensen, Cameron, Shawcross, Wilson, Muniesa, Whelan, Nzonzi, Odemwingie, Ireland, Arnautovic, Walters
Akiba: Pieters, Palacios, Adam, Crouch, Etherington, Wilkinson, Butland.
Refa: Lee Probert

MSIMAMO

POS
LP CLUB P W D L GF GA GD PTS
1 (1) Manchester City 38 27 5 6 102 37 65 86
2 (2) Liverpool 38 26 6 6 101 50 51 84
3 (3) Chelsea 38 25 7 6 71 27 44 82
4 (4) Arsenal 38 24 7 7 68 41 27 79
5 (5) Everton 38 21 9 8 61 39 22 72
6 (6) Tottenham Hotspur 38 21 6 11 55 51 4 69
7 (7) Manchester United 38 19 7 12 64 43 21 64
8 (8) Southampton 38 15 11 12 54 46 8 56
9 (10) Stoke City 38 13 11 14 45 52 -7 50
10 (9) Newcastle United 38 15 4 19 43 59 -16 49
11 (11) Crystal Palace 38 13 6 19 33 48 -15 45
12 (13) Swansea City 38 11 9 18 54 54 0 42
13 (12) West Ham United 38 11 7 20 40 51 -11 40
14 (14) Sunderland 38 10 8 20 41 60 -19 38
15 (15) Aston Villa 38 10 8 20 39 61 -22 38
16 (16) Hull City 38 10 7 21 38 53 -15 37
17 (17) West Bromwich Albion 38 7 15 16 43 59 -16 36
18 (18) Norwich City 38 8 9 21 28 62 -34 33
19 (19) Fulham 38 9 5 24 40 85 -45 32
20 (20) Cardiff City 38 7 9 22 32 74 -42 30
POS
LP CLUB P W D L GF GA GD PTS

No comments:

Post a Comment