Kocha wa Mabingwa wa Dunia Spain,Vincente Del Bosque, amechelewesha kutaja Kkosi chake cha mwisho cha
Wachezaji 23 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil na
badala yake amemwita Gerard Deulofeu, aliekuwa Everton kwa Mkopo, na
kuwaacha Wachezaji wa Real Madrid na Atletico Madrid kwa ajili ya Mechi
ya kujipima nguvu na Bolivia.
Ilitegemewa kuwa Leo hii Vincente Del
Bosque angelipunguza Kikosi chake kutoka Wachezaji 30 na kubakisha 23 tu
kama inavyotakiwa na FIFA kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia lakini
badala yake amewaita Wachezaji 19 tu kwa ajili ya Mechi ya Ijumaa Mei
30 na Bolivia.
Wachezaji wote wa Real na Atletico
waliokuwemo kwenye Kikosi cha Awali cha Wachezaji 30 hawakuitwa kwa
ajili ya Mechi na Bolivia na Vincente Del Bosque amesema: “Hatuhitajiki
kuwapa FIFA Listi ya Wachezaji 23 hadi Juni 2, sasa kwa nini tutangaze
sasa?”Uamuzi huu utawanufaisha sana Wachezaji Majeruhi kama vile Diego Costa wa Atletico Madrid na kuwapa muda zaidi wa kupona.
Lakini Mchezaji alienufaika sana ni
Kiungo wa Barceloana, Gerard Deulofeu, ambae Msimu huu alikuwa England
kwa Mkopo huko Everton hasa kwa vile yeye si mmoja wa Wachezaji 30
waliotangazwa awali.Del Bosque ameeleza: “Tunamwamini na hasa Wachezaji wakijitoa Kikosini yeye anafaa tu!Wachezaji wengine waliokuwemo kwenye
Kikosi cha Wachezaji 30 lakini wameachwa kwenye Mechi hii na Bolivia
itakayochezwa huko Seville ni pamoja na Wachezaji wawili wa Man City,
Jesus Navas na Alvaro Negredo, pamoja na Straika wa Juventus, Fernando
Llorente.
KIKOSI KILICHOITWA KUCHEZA NA BOLIVIA:
Pepe Reina, David De Gea, Gerard Pique,
Raul Albiol, Javi Martinez, Jordi Alba, Cesar Azpilicueta, Alberto
Moreno, Zavi Hernandez, Andres Iniesta, Sergio Busquets, Santi Cazorla,
Ander Iturraspe, Cesc Fabregas, Juan Mata, David Silva, Pedro Rodriquez,
Fernando Torres, Gerard Deulofeu.
No comments:
Post a Comment