Social Icons

Saturday 17 May 2014

Romelu Lukaku kutolewa Sadaka kwa Atletico Madrid


Klabu ya Chelsea imemtoa sadaka Romelu Lukaku kwa Atletico Madrid ikiwa ni sehemu ya juhudi zao za kutaka kumsajili Diego Costa. Costa ni mchezaji anayepewqa kipaumbele na kocha Jose Mourinho katika uasajili wa kiangazi na anataka biashara hiyo ikamilike haraka.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye anategemewa kuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwa ajili ya Kombe la dunai amefunga mabao 27 msimu huu na anakadiriwa ataigharimu Chelsea zaidi ya paundi milioni 32. Katika kuhakikisha dili hilo linakamilika Chelsea wamemtoa Lukaku kama italazimika wabadilishane ili kukamilisha usajili huo.

Lukaku mwenye umri wa miaka 21 alitua Chelsea kwa paundi milioni 18 akitokea Anderlecht mwaka 2011 na amefunga mabao 16 msimu huu akiwa kwa mkopo Everton lakini anaonekana bado hayupo katika mipango ya timu hiyo msimu ujao.

No comments:

Post a Comment