Mmiliki wa Aston Villa, Randy Lerner,
amesema umefika wakati muafaka kwa Klabu hiyo kutafuta njia mbadala
baada ya kuiweka Sokoni kuiuza Klabu hiyo.Lerner, ambae ni Mfanyabiashara wa
Kimarekani alieinunua Villa Mwaka 2006 kutoka kwa Doug Ellis ambae
aliimiliki Villa kwa muda mrefu, ameamua kuiuza Klabu hiyo baada Msimu
huu kumaliza ikiwa Nafasi ya 15 kwenye Ligi Kuu England.
MAN UNITED YATAFAKARI KUIKOSA ULAYA!
Ryan Giggs anaamini kukosa kucheza Mashindano ya UEFA Msimu ujao ni baraka kwa Manchester United.
Man United walimaliza Msimu huu Nafasi
ya 7 na hivyo kukosa kuwemo UEFA CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI kwa Msimu
ujao na hii ni mara ya kwanza tangu Msimu wa 1989/90 kwa Old Trafford
kuzikosa Mechi za Ulaya.Ingawa Giggs, ambae ni Meneja wa Muda wa
Man United, amekiri hilo litaathiri sana Wachezaji wasiokuwa na Namba
kwenye Timu kwa kukosa Mechi nyingi za kucheza, amebainisha kuwa pengine
hiyo ni baraka kwao kwa kucheza Mechi chache Msimu huo mpya na hivyo
kujiimarisha na kunufaika kwenye Ligi kama walivyonufaika Liverpool
Msimu huu.Giggs amesema: “Unaweza kutazama hilo
kwa namna tofauti. Tuna Kikosi kikubwa na baadhi ya Wachezaji wanaweza
kukosa nafasi za kucheza kama tupo nje ya Ulaya lakini ikiwa
tutafanikiwa kwenda mbali kwenye Vikombe vya England hilo litawasaidia!”
TETESI: CHIPUKIZI SOUTHAMPTON:LALLANA LIVERPOOL, LUKE SHAW MAN UNITED!
KIUNGO wa Southampton, Adam Lallana,
mwenye Miaka 26, na mwenzake Fulbeki Luke Shaw, Miaka 18, ambao wote
wameteuliwa Kikosi cha Wachezaji 23 cha England kwa ajili ya Fainali za
Kombe la Dunia huko Brazil, inasemekana wako mbioni kuhamia Liverpool na
Manchester United.
Inasadikiwa Liverpool imeshatoa Ofa kumnunua Lallana na Man United wamebwaga Dau la Pauni Milioni 27 kumnasa Shaw. Mwenyekiti wa Southampton, Ralph
Krueger, ameshasema kwamba Mastaa wao wako mbioni kuhamia Klabu Vigogo
za England na wao wapo wazi kuzungumza na yeyote yule.
No comments:
Post a Comment