Social Icons

Thursday 8 May 2014

LIGI KUU ENGLAND inamalizika Jumapili huku Bingwa wa kumrithi Manchester United


LIGI KUU ENGLAND inamalizika Jumapili huku Bingwa wa kumrithi Manchester United bado kupatikana ingawa Jirani yake Manchester City ndie mwenye nafasi kubwa kulibakisha Kombe Jijini Manchester.
Man City wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 2 mbele ya Liverpool na pia wana Tofauti ya Magoli Bora wakiwa na Goli 13 mbele ya Liverpool na hayo yote yanaifanya City wahitaji ushindi na hata Sare itawapa Taji watakapocheza Nyumbani kwao Etihad na West Ham ambayo inakamilisha Ratiba tu.Liverpool wao wako Nyumbani kwao Anfield kucheza na Newcastle na wanatakiwa washinde na kusali Man City ifungwe ili watwae Ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 24.


Mbali ya kutojulikana nani Bingwa pia bado haijaulikana Timu gani itamaliza Nafasi ya 6 na kucheza EUROPA LIGI ingawa Tottenham ndio wenye nafasi kubwa kwani Sare tu kwao itawahakikishia hilo lakini wakifungwa tu na Man United kushinda basi Man United watachukua nafasi hiyo kucheza EUROPA LIGI.
Kwenye kushuka Daraja, tayari Timu 2, Cardiif City na Fulham, zimeshateremka tangu Wikiendi iliyopita na bado Timu moja lakini Norwich City ndio wenye uhakika mkubwa wa kuporomoka kwani kubaki kwao itakuwa miujiza mikubwa sana kwa vile, kwanza wanahitaji kushinda na pili West Bromwich Albion wafungwe lakini hayo pia hayatoshi kwani Matokeo hayo yanahitaji yaambatane na mabadiliko ya Tofauti ya Magoli kubwa sana.

WBA wana Pointi 36 na Tofauti ya Magoli -15 na Norwich wana Pointi 33 na Tofauti ya Magoli -32 na hivyo kufungwa kwa WBA na kushinda kwa Norwich lazima kubadilishe Tofauti ya Magoli kwa idadi ya Goli 17.




Zile Timu 4 za kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao tayari zimepatikana na ambazo ni Man City, Liverpool, Chelsea na Arsenal lakini Arsenal, kwa kumaliza Nafasi ya 4, itabidi waanze hatua ya awali ya Mechi za Mchujo.Tayari FA, Chama cha Soka England, kimeshatangaza Marefe kwa ajili ya Mechi hizo 10 za mwisho za Ligi Kuu England.

Ligi hii itaanza Msimu mpya hapo Agosti 17 na Wiki moja kabla itachezwa ile Mechi ya Fungua Pazia Msimu mpya wa 2014/15 ambapo Bingwa wa Ligi Kuu England atapambana na Bingwa wa FA CUP Uwanjani Wembley Jijini London.

LISTI KAMILI YA MAREFA:
-Manchester City vs West Ham United: Martin Atkinson
-Liverpool vs Newcastle United: Phil Dowd
-Tottenham vs Aston Villa: Jon Moss
-West Brom vs Stoke City: Lee Probert
-Southampton vs Manchester United: Mike Dean
-Fulham vs Crystal Palace: Kevin Friend
-Hull City vs Everton: Howard Webb
-Cardiff City vs Chelsea: Michael Oliver
-Norwich City vs Arsenal: Lee Mason
-Sunderland v Swansea City: Chris Foy

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Mechi za Mwisho za Msimu
Jumapili 11 Mei 2014
[Mechi zote Saa 1100 Jioni, Saa za Tanzania]
Cardiff v Chelsea
Fulham v Crystal Palace
Hull v Everton
Liverpool v Newcastle
Man City v West Ham
Norwich v Arsenal
Southampton v Man United
Sunderland v Swansea
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Stoke

No comments:

Post a Comment