KLABU ya Paris
Saint-Germain-PSG wametawadhwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini
Ufaransa baada ya Monaco kung’ang’ania sare na timu iliyo katika hatari
ya kushuka daraja ya Guingamp.
Manaco walikuwa wakijua kuwa wanatakiwa
kushinda mchezo huo ili kuweka matumaini yao finyu ya ubingwa hai. Kwa
matokeo PSG ambao wanajitupa uwanjani baadae kumenyana na Rennes
watakwenda katika mchezo huo huku tayari wakijijua mabingwa.
No comments:
Post a Comment