Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta nchini
Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na
viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo
wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa
muda mfupi.
“Badala ya wanachama kuja Dar es salaam makao
makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya hivyo popote
walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae
kupewa kadi ya uanachama” alisema Deo.
Gharama za kujiunga na uanchama zitabakia
zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo
mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake ambayo
pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na kutoa
fedha.
Naye Makaumu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga
Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kufikia
makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza kujua idadi
ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu zitaweza
kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za uanachama
utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la
Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja kwa moja
zoezi la kuhamisha wanachama kutoka kwenye mfumo wa analogy kwenda
digital utaanza.
No comments:
Post a Comment