MCHEZAJI BORA DUNIANI,Cristiano Ronaldo, yuko mbioni kutwaa‘Pichichi’ambayo ndio Tuzo ya Mfungaji Bora wa La Liga inayotolewa na Jarida la Marca.Juzi Ronaldo alifunga Bao safi, murua na
la Msimu alipoisawazishia Real Madrid katika Dakika za Majeruhi
walipotoka 2-2Uwanjani Santiago Bernabeu na Valencia na hilo ni Bao
lake la 50 Msimu huu na ni Bao la 31 kwenye La Liga.
Ronaldo ndie anaongoza kwa Ufungaji Bora
La Liga akiwa na Bao 31, zikiwa Bao 3 mbele ya Lionel Messi wa
Barcelona na 4 mbele ya Diego Costa wa Atletico Madrid lakini Ronaldo
ana nafasi kubwa ya kupiga Bao zaidi kwa vile Real wamebakisha Mechi 3
za La Liga na Barca na Atletico wana Mechi 2 kila mmoja.
Cristiano Ronaldo: Takwimu Msimu wa 2013/2014:
MAGOLI: 50
LA LIGA: 31
Copa del Rey: 3
UEFA Champions League: 16
Mechi za Kujipima kabla Msimu kuanza: 6
NAMNA YALIVYOFUNGWA:
-Kichwa: 5
-Frikiki: 5
-Penati: 9
-Mguu wa Kulia: 25
-Mguu wa Kushoto: 6
MAMBO MUHIMU:
-PICHICHI hutolewa na Jarida la Marca kwa Mfungaji Bora wa La Liga
-Kwa Makipa, Kipa anaeokoa Michomo mingi hutunukiwa Tuzo ya Ricardo Zamora.
-WASHINDI wa hivi karibuni wa PICHICHI:
Lionel Messi 2013
Lionel Messi 2012
Cristiano Ronaldo 2011
Lionel Messi 2010
Diego Forlán 2009
-WAFUNGAJI BORA LA LIGA:
1 Cristiano Ronaldo Real Madrid 31
2 Lionel Messi Barcelona 28
3 Diego Costa Atletico 27
4 Alexis Sánchez Barcelona 18
5 Karim Benzema Real Madrid 17
No comments:
Post a Comment