Social Icons

Sunday 22 June 2014

Dakika 90 za Mchezo Kati ya Ghana Na Ujerumani Tazama Hapa Magoli


Miroslav Klose aliinusuru Germany kipigo na pia kufikisha Rekodi ya Ronaldo ya Bao 15 za Magoli kwemyeFainali za Kombe la Dunia baada Jana kuisawazishia huko Estadio Castelao, Jijini Fortaleza Nchini Brazil na kutoka Sare 2-2 na Ghana kwenye Mechi ya Kundi G.


MAGOLI:Germany 2-Mario Götze Dakika ya 51-Miroslav Klose 71Ghana 2-Andre Ayew Dakika ya 54 -Asamoah Gyan 63....Germany na Ghana zitacheza Mechi zao za mwisho hapo Alhamisi Juni 26 kwa Germany kucheza na USA na Ghana kuivaa Portugal.



 Leo Usiku ipo Mechi nyingine ya Kundi G kati ya Portugal na USA.

NIGERIA YAIFUNGA BOSNIA 1-0!


WAKICHEZA huko Arena Pantanal, Mjini Cuiaba Nchini Brazil, Nigeria Jana waliifunga Bosnia-Herzegovina Bao 1-0 katika Mechi ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia.Bao hilo muhimu lilifungwa na Peter Odemwingie katika Dakika ya 29 na kuweka matmaini ya Nigeria kutinga Raundi ya Pili.

No comments:

Post a Comment