Social Icons

Wednesday, 7 May 2014

VAN GAAL akubari dili kuwakoha MANCHESTER UNITED


Louis van Gaal amefikia makubaliano kuwa Meneja mpya wa Manchester United kwa mujibu wa duru za habari za ndani huko Egland.Hata hivyo, Klabu ya Man United imedokeza kuwa haitatangaza habari yeyote kuhusu Meneja mpya Wiki hii.Van Gaal ndie Kocha wa Timu ya Taifa ya Netherlands ambayo Mwezi Juni itakuwa huko Brazil kucheza Fainali za Kombe la Dunia.Habari hizo kuhusu Mdachi huyo kukubali kuwa Meneja mpya pia zimethibitisha kuwa Meneja wa sasa wa Muda, Ryan Giggs, ambae aliteuliwa mara tu baada ya kufukuzwa David Moyes, atabaki na kuwa mmoja wa Makocha chini ya Louis van Gaal.

Van Gaal, Miaka 62, ameshatwaa Ubingwa kwenye Ligi za Holland, Spain na Germany akiwa na Klabu za Ajax, Barcelona and Bayern Munich na pia kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 1995 akiwa na Ajax.Inatarajiwa Van Gaal ataijenga upya Man United kwa kusajili Wachezaji wapya kadhaa kabla Msimu mpya wa 2014/15 kuanza hapo Agosti 17.

WASIFU:
Jina Kamili: Aloysius Paulus Maria van Gaal
Kuzaliwa: 8 August 1951 (age 62)
Mahali: Amsterdam, Netherlands
Uchezaji, Pozisheni: Kiungo
Kazi ya sasa: Meneja Timu ya Taifa Netherlands
Timu ya Vijana: RKSV de Meer

Klabu:
(Kwenye Mabano Magoli)
1972–1973   Ajax Mechi 0 (0)
1973–1977   Royal Antwerp Mechi 43 (7)
1977–1978   Telstar Mechi 25 (1)
1978–1986   Sparta Rotterdam Mechi 248 (26)
1986–1987   AZ Mechi 17 (0)
Jumla: Mechi 333 (34)

Umeneja:
1986–1988   AZ (Msaidizi)
1988–1991   Ajax (Msaidizi)
1991–1997   Ajax
1997–2000   Barcelona
2000–2002   Netherlands
2002–2003   Barcelona
2005–2009   AZ
2009–2011   Bayern Munich
2012– Netherlands

Mataji kama Meneja
AJAX
Eredivisie: 1993–94, 1994–95, 1995–96
KNVB Cup: 1992–93
Johan Cruijff Shield: 1993, 1994, 1995
UEFA Champions League: 1994–95
UEFA Cup: 1991–92
UEFA Super Cup: 1995
Intercontinental Cup: 1995

BARCELONA
La Liga: 1997–98, 1998–99
Copa del Rey: 1997–98
UEFA Super Cup: 1997

AZ
Eredivisie: 2008–09
Bayern Munich
Bundesliga: 2009–10
DFB-Pokal: 2009–10
DFB-Supercup: 2010
Tuzo Binafsi
World Soccer Manager of the Year: 1995
Onze d'Or Coach of the Year: 1995
Rinus Michels Award: 2007, 2009
Dutch Sports Coach of the Year: 2009
Die Sprachwahrer des Jahres (3rd place): 2009
German Football Manager of the Year: 2010

No comments:

Post a Comment