Social Icons

Saturday 21 June 2014

Huko Brazili Leo Argentina Kukutana na Wataalamu wa Nyuklia,Ghana Kuvaana na Wajerumani,Nigeria v Bosnia-Herzegovina Tazama Hapa Hali Za Vikosi


Ghana Leo huko Brazil wanaingia kwenye Mechi yao ya Pili ya Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia kucheza na Germany.Kwenye Mechi ya Kwanza,
 

Ghana walipoteza 2-1 na USA na Germany kuitwanga Portugal Bao 4-0.Mechi nyingine ya Kundi G itachezwa Jumapili kati ya USA na Portugal.Germany wataingia kwenye Mechi huku Straika wao Thomas Muller, ambae ndie alitwaa Buti ya Dhahabu huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010, akiwa moto kwani tayari ana Bao 3 baada ya kupiga Hetitriki walipoibamiza Portugal 4-0.
Walipocheza na USA, Ghana walipata pigo mwanzoni wakati Clint Dempsey alipofunga Bao kwa USA Sekunde 30 tu tangu Mechi ianze lakini Andre Ayew akasawazisha Dakika ya 82 na USA kufunga Bao la ushindi kupitia Brooks Dakika ya 87.
Hii ni Mechi inayoweza kushuhudia kwa Ndugu wawili kucheza wakati Ghana inaweza kuwapanga Jordan Ayew na Kaka yake Andre Ayew, wote wakichezea Klabu ya Olympique de Marseille ya France, na pia kumchezesha Kevin-Prince Boateng, anaechezea Schalke huko Germany, ili akabiliane na Kaka yeke Jerome Boateng ambae yuko Timu ya Taifa ya Germany.Jerome Boateng huchezea Bayern Munich.

NDUGU

MSIMAMO:
KUNDI G
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Germany
1
1
0
0
4
0
4
3
United States
1
1
0
0
2
1
1
3
Ghana
1
0
0
1
1
2
-1
0
Portugal
1
0
0
1
0
4
-4
0

Katika Historia yao ya Fainali za Kombe la Dunia, Ghana hawajawahi kushindwa kufuzu kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano lakini wakifungwa Mechi hii na Germany basi huenda Rekodi hiyo ikavunjwa.Huko Afrika Kusini Mwaka 2010, Ghana na Germany zilikutana kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Germany kuibuka Mshindi kwa Bao la Mesut Ozil.

VIKOSI VINATARAJIWA:
GERMANY: Neuer; Boateng, Howedes, Mertesacker, Hummels; Lahm, Khedira, Kroos, Ozil, Gotze; Muller
GHANA: Larsen Kwarasey; Opare, Asamoah, Boye, Mensah; Muntari, Atsu, Rabiu, J.Ayew, A.Ayew; Gyan


REFA: Sandro RICCI [Brazil]
 Iran wakishangilia goli lao

KOMBE LA DUNIA
RATIBA
JUMAMOSI, JUNI 21, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina v Iran
F
Estadio Mineirão
2200
Germany v Ghana
G
Estadio Castelão
0100
Nigeria v Bosnia-Herzegovina
F
Arena Pantanal


 Argentia wakishangilia
JUMAPILI, JUNI 22, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Belgium v Russia
H
Estadio do Maracanã
2200
South Korea v Algeria
H
Estadio Beira-Rio
0100
United States v Portugal
G
Arena Amazonia


Nigeria Leo huko Brazil wanaingia kwenye Mechi yao ya Pili ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia kucheza na Bosnia-Herzegovina.Kwenye Mechi ya Kwanza, Nigeria walitoka 0-0 na Iran na Bosnia kuchapwa 2-1 na Argentina.Mapema hii Leo, huko Estadio Mineirão, Argentina watacheza na Iran.


 Kikosi cha Nigeria Mazoezini
Nigeria na Bosnia hazijawahi kukutana kabla na Nigeria wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajashinda hata Mechi moja kwenye Mechi zao 9 zilizopita za Fainali za Kombe la Dunia.Lakini Bosnia wanaingia Uwanjani wakijawa na matumaini makubwa baada ya kuiendesha mchakamchaka Argentina, moja ya Timu inayopewa nafasi ya Ubingwa wa Dunia, ambao waliifunga Bosnia 2-1 kwa Goli la kujifunga wenyewe la Sead Kolasinac na ‘uchawi’ wa Lionel Messi kuwapa ushindi.
 Bosnia-Herzegovina Wakiwa mazoezini

MSIMAMO:
KUNDI F
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Argentina
1
1
0
0
2
1
1
3
Iran
1
0
1
0
0
0
0
1
Nigeria
1
0
1
0
0
0
0
1
Bosnia
1
0
0
1
1
2
-1
0

Leo hii, Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi, anaweza kuwaanzisha wazoefu Shola Ameobi na Peter Odemwingie kwenye Fowadi ili kusaka ushindi kuhimu.

VIKOSI VINATARAJIWA:
NIGERIA (Mfumo: 4-2-3-1):
Vincent Enyeama;Juwon Oshaniwa, Joseph Yobo, Kenneth Omeruo; Efe Ambrose;Ogenyi Onazi, John Obi Mikel; Victor Moses,Ramon Azeez, Ahmed Musa;Emmanuel Emenike.

BOSNIA AND HERZEGOVINA (Mfumo: 4-2-3-1):
Asmir Begović;Sead Kolašinac, Emir Spahić, Ermin Bičakčić, Mensur Mujdža;
Muhamed Bešić, Miralem Pjanić; Senad Lulić,Zvjezdan Misimović, Izet Hajrović;
Edin Džeko.

REFA: Peter O LEARY [New Zealand]

No comments:

Post a Comment