Social Icons

Sunday 22 June 2014

Kombe la Dunia Mchezaji wa Miaka 19, Divock Origi Aipeleka Belgium Raundi ya Pili


Mchezaji wa Miaka 19, Divock Origi, akitokea Benchi, alifunga Bao zikiwa zimesalia Dakika 2 na kuiingiza Belgium Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil baada ya kuifunga Russia Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kundi H.






Kipindi cha Kwanza Russia walikosa nafasi ya wazi pale Alexander Kokorin alipopiga Kichwa nje lakini pia Belgium walikosa Bao zikiwa zimebaki Dakika 7 baada ya Shuti la Kevin Mirallas  kugonga Posti.Lakini kazi safi ya Eden Hazard kumlisha Origi ndio iliwapa ushindi Belgium na kuwaingiza Raundi ya Pili.


No comments:

Post a Comment