Social Icons

Thursday 26 June 2014

Baada Ya Ander Herrera, ripoti zimevuja kuwa Luke Shaw anapimwa afya Klabuni Manchester United


Baada Leo rasmi kumchukua Kiungo kutoka Klabu ya Spain Athletic Club Bilbao, Ander Herrera, ripoti zimevuja kuwa Fulbeki Chipukizi wa England Luke Shaw anapimwa afya Klabuni Manchester United tayari kukamilisha taratibu za kujiunga.


Shaw, Beki wa Miaka 18 anaechezea Southampton, ndio kwanza amerudi na Kikosi cha England kilichokuwa huko Brazil na kutolewa nje ya Kombe la DuniaUhamisho wa Luke Shaw huenda ukamfanya awe Chipukizi wa Bei kali alieuzwa katika Historia ya Uingereza kwani Dau lake linakisiwa kukaribia Pauni Milioni 30. 

Mwezi Mei, Man United walitoa Ofa ya Psuni Milioni 27 kumnunua na kukataliwa na Southampton.Shaw, ambae atatimiza Miaka 19 Jula 12, ameshacheza Mechi 60 za Ligi Kuu England akiwa na Southampton na Mechi 3 na Timu ya Taifa ya England ambako alimpokonya namba mkongwe Ashley Cole.

Ingawa Man United imemuongezea Mwaka mmoja Fulbeki wa Kushoto Patrice Evra lakini inaaminika Meneja mpya Louis van Gaal atakuwa akimtumia Shaw zaidi wakati Mchezaji mwingine wa nafasi hiyo, Alexander Buttner, akielekea Dinamo Moscow.

No comments:

Post a Comment