Social Icons

Saturday 21 June 2014

Hali Bado ni Tete Huko Nigeria, shambulio jingine limetokea Karibu na kijiji Walichotekwa Wasichana

Ripoti zinasema kuwa shambulio jengine limetokea katika kijiji kimoja cha kaskazini-mashariki mwa Nigeria, karibu na pahala ambapo wasichana wa shule zaidi ya mia-mbili walitekwa nyara.


  
Kiongozi mmoja wa kijiji Amesema kwamba watu waliokuwa na silaha walivamia kijiji cha Koronginim, kama kilomita 14 kutoka Chibok ambako wasichana walitekwa na wapiganaji Waislamu wa kundi la Boko Haram mwezi Aprili.

Alieleza kuwa watu kama watatu waliuwawa na kwamba kijiji hicho kimeteketezwa na moto.Aliongeza kusema anafikiri washambuliaji walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.

No comments:

Post a Comment