Social Icons

Thursday 19 June 2014

Taarifa Juu Ya Jambazi Mmoja Kuuwawa Mkoani Mbeya


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limeua jambazi Joseph Kapinga Mkazi wa Mafiga Mkoani Morogoro akiwa na silaha aina ya Ak 47 yenye risasi 25 kwenye magazine.Tukio hilo limetokea June 19 mwaka huu majira ya saa 11 alfajili ambapo askari polisi walikutana na watu waliowatilia shaka kutokana na jinsi walivaa.




Akizungumza na waandishi wa habari jiji hapa Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa majambazi hao waliarifiwa na walinzi wa soko kuu la Tunduma .Amesema mara baada ya kupata taarifa hizo askari waliokuwa doria walianza msako mkali wa kuwatafuta watu hao.





No comments:

Post a Comment