Social Icons

Saturday 14 June 2014

Kombe La Dunia Leo Huko Brazil Macho Ya Wengi Kutazama England Vs Italy,,Leo Uruguay kuivaa Costa Rica ...Tazama Hali Za Vikosi Hapa


Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Usiku Wa Leo zinaanza Mechi zao za kwanza kwa Uruguay kuivaa Costa Rica huko Estadio Castelão Jijini Fortaleza na kufuatia ule mtanange unaongojewa kwa hamu, England v Italy.




TAARIFA ZA WACHEZAJI/TATHMINI/REKODI/VIKOSI:
Hali za Wachezaji
Fowadi wa England Danny Welbeck amepona tatizo lake la enka lakini Alex Oxlade-Chamberlain bado hajapona maumivu ya Goti lake aliloumia walipocheza Mechi ya Kirafiki na Ecuador huko Marekani Wiki 2 zilizopita.Italy huenda wakalazimika kutumia Masentahafu wa 3 nyuma badala ya kusimamisha Difensi ya Mtu 4 baada ya Fulbeki wao Mattia De Sciglio kuumia Pajani.Lakini habari njema kwa Italy ni zile za Mario Balotelli na Marco Verratti kupata afueni matatizo yao kiafya.

England National Team

Tathmini
Matumaini ya England ya mafanikio kwenye Mechi za Kimataifa yanaanza na Kikosi cha Cesare Prandelli, Italy, ambacho ndicho kilichowatoa kwenye Mashindano ya mwisho makubwa huko kwenye michuano ya EURO 2012 walipobwagwa kwa Mikwaju ya Penati.Kila Timu inatinga ndani ya Arena Amazônia Jijini Manaus ikihofia athari za Joto na hivyo watacheza Soka la tahadhari la kumiliki Mpira ili wasiupoteze ovyo na kupoteza nguvu ovyo kwa kuukimbiza kutaka kuumiliki tena. 

Italy National Team

Kama ilivyokuwa kwenye EURO 2012, Mpishi mkuu wa Italy ni Mkongwe Andrea Pirlo, ambae sasa ana Miaka 35, na ambae huko Kiev Miaka minne iliyopita alitoa Pasi nyingi kupita Wacheza wote wa Kiungo wa England na kuzunguka umbali mrefu kupita Mchezaji yeyote wa England kwenye Mechi hiyo ya EURO 2012.

Mario Balotel

Lakini England ya hivi sasa, chini ya Meneja Roy Hodgson, ni ya Chipukizi wengi, kina Daniel Sturridge, Raheem Sterling na Ross Barkley, wakiongezwa nguvu na Wakongwe Steve Gerrard, Frank Lampard na Wayne Rooney.

Wayne Rooney.

Uso kwa Uso
-Jumla Mechi 24
-England: Ushindi Mechi 8 Magoli: 30
-Sare: 7
-Italy: Ushindi 9 Magoli: 27

Dondoo muhimu
-Mara pekee kwa England na Italy kukutana kwenye Kombe la Dunia ni kwenye Mechi ya kuwania Mshindi wa Tatu Mwaka 1990 ambayo Italy walishinda 2-1.
-England wameshinda Mechu 2 tu kati ya 11 walizocheza mwisho dhidi ya Italy wakifungwa 6.
-Mara ya mwisho kukutana ilikuwa huko Switzerland Mwezi Agosti Mwaka 2012 na England kushinda 2-1.

VIKOSI VINAVYOTARAJIWA:
England: Hart, Johnson, Jagielka, Cahill, Baines, Gerrard, Henderson, Lallana, Sterling, Rooney, Sturridge

Italy: Buffon, Abate, De Sciglio, Bonucci, Chiellini, De Rossi, Pirlo, Verratti, Candreva, Marchisio, Balotelli

REFA: Bjorn Kuipers [Holland]

No comments:

Post a Comment