Timu hizo mbili zilitoka sare bila kufangana
bao lolote, huku Ugiriki ikimaliza mechi hiyo na wachezaji kumi baada ya
nahodha wao kutimuliwa mchezoni.Kundi lao laongozwa na Colombia na alama 6 nayo Ivory Coast ni ya pili kwa alama 3.
Muda mfupi baadaye nahodha wa Ugiriki, Konstantinos Katsouranis, alionyeshwa kadi ya manjano kwa mara ya pili na akaondoka mchuanoni baada ya kumchezea vibaya nahodha wa Japan Makoto Hasebe.

Kuondolewa kwake kulitia moto katika kikosi cha
Ugiriki na walionekana kuonyesha mchezo mzuri wakiwa wachezaji 10 kuliko
walivyokua 11.Vasileios Torosidis , alitoamwakju safi iliyomlakimu kipa wa Japan, Eiji Kawashima kufanya kazi ya ziada.
Georgios Samaras pia alijaribu bahati yake kutoka kwa mpira wa adhabu nao ukampita Kawashima ila tu ulielekea nje.Kikosi hicho cha Fernando Santos kilizidi
kushambulia na katika kipindi cha pili, Mchezaji wa akiba Theofanis
Gekas aliugonga kwa kichwa mpira wa kona lakini ukaokolewa na kipa wa
Japan.
Samurai Blue wa Japan waliamka pia katika dakika
ya 68 pale ambapo Atsuto Uchida alipompa Yoshito Okubo mpira ila tu
Okubo aliupiga nje.Uchida pia akaijaribu safu ya ulinzi ya Ugiriki na mpira wake pia ukaelekea nje.Japan ilimaliza mechi hiyo ikionekana kuwa yenye
nguvu zaidi ya Ugiriki, Hata hivyo, ili kupata matumaini ya kuendelea,
wanatarajiwa kukishinda kikosi cha Colombia kinachoongoza kundi hilo la
sivyo ivory coast itamaliza katika nafasi ya pili.
Ivory coast imeratibiwa kuchuana na Ugiriki
katika mechi yao ya mwisho ambayo sasa wanahitaji ushindi
ilikujihakikishia nafasi ya pili nyuma ya Colombia ambayo tayaari
imeshafuzu kwa mkondo ujao.
No comments:
Post a Comment