Social Icons

Friday 27 June 2014

Ukraine, Georgia na Moldova zimetia sahihi mikataba ya ushirikiano na muungano wa ulaya


Ukraine, Georgia na Moldova zimetia sahihi mikataba ya ushirikiano na muungano wa ulaya, swala ambalo Urusi inapinga vikali.Makubaliano hayo ambayo yatayaunganisha pamoja mataifa hayo na kuyaegemeza Magharibi kiuchumi na kisiasa, haswa ndio msingi wa mgogoro ulioko Ukraine.


Usitishaji wa vita kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaounga mkono Urusi, mashariki mwa Ukraine, unakamilika Ijumaa hii.Urusi imesema kuwa hata ingawa kutia saini mkataba huo ni haki ya taifa lolote, kunaweza kuleta madhara mabaya baadaye.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko aliusifu mkataba huo akisema ni siku ya kihistoria katika taifa la Ukraine baada ya siku ya Uhuru wa taifa hilo mwaka 1991.
Ameutaja kuwa dalili ya imani na nia isiyoweza kuvunjwa.
Poroshenko pia amesema kuwa ameuona mkataba huo kama mwanzo wa mchakato wa kujiunga na Umoja wa bara Uropa,''Ukraine inadhibitisha chaguo lake la kitaifa, kujiunga na EU" alisema.
Kwengineko, rais wa Umoja wa bara Uropa, Herman va Rompuy ametaja kuwa "siku kuu kwa bara Uropa".
''Umoja wa bara Uropa unasimama pamoja nanyi, leo zaidi ya siku nyingine yoyote awali" aliwaambia viongozi wa nchi hizo tatu, akiongeza kuwa hakuna chochote katika mikataba hiyo ya makubaliano kitakachoiletea madhara Urusi kwa njia yoyote ile.

Rais Poroshenko akitia sahihi makubaliano ya ushirikiano na ulaya.

Naibu waziri wa maswala ya nje wa Urusi, Grigory Karasin ''ameliambia shirika la habari la Interfax kuwa hatua hiyo huenda ikazua madhara.Kutiwa sahihi kwa mkataba huu muhimu, kwa hakika ni haki ya taifa lolote lile" alisema.
Ila tu matokeo ya Ukraine na Moldova kutia saini mkataba huu bila shaka yatakuwa mabaya".
Mapema, mshauri mkuu wa Kremlin, Sergei Glazyev alimtaja Poroshenko kuwa mwanachama wa Nazi na kuwa uchaguzi wake kuwa rais haukuwa wa haki kwani sehemu kubwa ya Ukraine haikupiga kura katika uchaguzi wa mwezi Mei.

Alizidi kusema kuwa Poroshenko hana haki kikatiba kutia sahihi mkataba huo, jambo ambalo litadhuru uchumi wa Ukraine.

No comments:

Post a Comment