Social Icons

Saturday 28 June 2014

Kombe La Dunia Pambano lao Leo Brazil Vs Chile Refa Howard Webb Ahofiwa na Chile


Kambi ya Brazil imechukizwa na kampeni ya Chile ya kutaka kumpa presha Refa kutoka England, Howard Webb, ambae ndie atakaechezesha pambano lao la Leo la Raundi ya Mtoano ya imu 16 huko Estadio Mineirao, rasmi kama Estádio Governador Magalhães Pinto, Jijini Belo Horizonte.
Watu kadhaa wa Timu ya Chile, akiwemo Straika Alexis Sánchez, wamesema wana wasiwasi na uchezeshaji wa Marefa.

Mchecheto wao unakuja kufuatia madai ya kichinchini kuwa Waamuzi wamekuwa wakiipendelea Brazil na kunyooshea kidole Penati waliyopewa Brazil walipocheza na Croatia baada ya Fred kuangushwa na pia Bao la Straika huyo huyo dhidi ya Cameroon kukubaliwa kukiwa na madai ni Ofsaidi.

Chile pia walimlalamikia Refa kutoka Gambia Bakary Gassama aliechezesha walipofungwa 2-0 na Holland kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi B Jumatatu iliyopita.Alexis Sanchez amesema: “Ninafurahi sana kucheza dhidi ya Brazil lakini kitu kinachonipa wasiwasi mkubwa ni uchezeshaji wa Marefa!” 

Hii itakuwa mara ya pili mfululizo Howard Webb kuichezesha Brazil na Chile kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Kombe la Dunia kwani Mwaka 2010 huko Afrika Kusini alichezesha Mechi hii hii na Brazil kuinyuka Chile Bao 3-0 na kulikuwa hamna manung’uniko yeyote.


Mwandishi wa Chile alijaribu kuliingiza swali la Marefa kwenye Mahojiano ya Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari akiwa na Nahodha wake Thiago Silva, na Wanahabari lakini Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Brazil, Rodrigo Paiva, aliingilia kati na kujibu: “Tutaongelea hili mara moja tu. Wanahabari huko Chile wamesisitiza suala hili Wiki yote sasa na hiki ni kitu hakistahili. Hii ni presha ya kipuuzi.”

Aliongeza: “Kuongelea hili si kuvunja heshima kwa FIFA, kwa Refa au kwa Timu ya Taifa ya Brazil, ‘Selecao’ au Watu wanaofanya kazi hapa kwa bidii kubwa, kwa Nchi yenye Historia ya Soka ya Miaka 100, Historia ya ushindi, hii ni kuvunjia heshima kwa Watu wa Brazil. Brazil haihitaji Refa kushinda Mechi na lazima uwaheshima ‘Selecao’ na Watu wa Brazil!’’

Uso kwa Uso
-Brazil na  Chile zimekutana mara 68 na Brazil kushinda 48, Chile 7, Sare 13
-Brazil imeifunga Chile Bao 159-58
-Kwenye Kombe la Dunia, Raundi za Mtoano, Brazil na Chile zimekutana mara 3 na zote Brazil kushinda. Mwaka 1962, kwenye Nusu Fainali, Brazil ilishinda 4-2. Mwaka 1998, Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Brazil walishinda 4-1 na huko Afrika Kusini, Mwaka 2010 pia Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Brazil ilishinda 3-0.

VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil: Cesar; Dani Alves, Thiago Silva, David Luiz, Marcelo; Paulinho, Luiz Gustavo; Willian, Oscar, Neymar; Fred
Chile: Bravo; Isla, Medel, Jara, Mena; Gutierrez, Aranguiz, Diaz, Valdivia; Sanchez, Vargas
REFA: Howard Webb [England] 

No comments:

Post a Comment