Social Icons

Thursday 26 June 2014

Mbrazil,Marcio Marcel Maximo,Ametua Jijini Dar es Salaam Tayari kujiunga na Klabuya Yangu.


Aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania anaetoka Brazil,Marcio Marcel Maximo, ametua Jijini Dar es Salaam mbioni kujiunga na Klabuya Yangu.Maximo, ambae amekuja na Ndege ya Shirika la Ndege ya Afrika Kusini, ameambatana na Msaidizi wake Leonadro Martins Neiva na alilakiwa na umati mkubwa wa Wana Yanga.


Viongozi wa Yanga waliokwenda kumlaki waliongozwa na Katibu Mkuu, Beno Njovu.Inatarajiwa Kesho Kocha Maximo ataongea na Wanahabari Makao Makuu ya Yanga Mitaa ya Jangwani na Twiga kuanzia Saa 5 Asubuhi.Kuhus ujio wake Tanzania kujiunga na klabu ya Yanga SC Maximo alisema kesho ataongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani majira ya saa 5 kamili asubuhi ambapo ndipo atapata fursa ya kueleza kila kitu juu ya ujio wake. 

Maximo alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza Mwaka 2006 kama Kocha wa Timu ya Taifa ambapo aliletwa kwa jitihada za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kudumu hadi 2010 na kuleta mapinduzi na mafanikio makubwa ikiwemo kucheza Fainali za CHAN.Wakati huo huo, Yanga imetangaza kuja kwa Kiungo Mshambuliaji kutoka Brazil Andrey Macrcel Ferreira Coutinho ambae anategemewa kutua Kesho Saa 8 Mchana ili kujiunga na Klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment