Social Icons

Friday 20 June 2014

Watendaji Wa Afya Watakao Husika na Wizi Wa Dawa na Fedha Kufukuzwa Kazi na Kufikishwa Kortini


Serikali imesema imeanza kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi na kuwafikisha mahakamani watendaji wa idara na sekta ya afya wanaotumia vibaya rasilimali fedha na watakaohusika na wizi pamoja na upotevu wa dawa,zinazotolewa na mashirika na wadau wa maendeleo wakishirikiana na serikali.


Akifungua mkutano mkuu wa kimkakati wa waratibu wa afya ya uzazi na mtoto wa kanda na mikoa yote nchini unaofanyika mjini Dodoma,naibu waziri na ustawi wa jamii Dkt KEBWE STEVEN KEBWE ,amesema pamoja na jitihada za serikali za kufikisha fedha na dawa katika hospitali na vituo vya afya nchini,bado kuna baadhi ya watendaji wanajinufaisha na rasilimali za umma kwa maslahi yao binafsi..


Pamoja na jitihada za serikali kufikisha dawa na fedha katika hospitali,zahanati na vituo vya afya,ili kuhakikisha lengo la millennia namba nne la kupunguza vifo vya mama na mtoto,linavukwa,imebainika kuwa bado mzimu wa wizi wa dawa ungali unasumbua kwa baadhi ya mikoa.

No comments:

Post a Comment