Social Icons

Thursday 19 June 2014

Mkuu wa SABC Adaiwa Kupewa Mke Kama Zawadi


Serikali ya Afrika Kusini imeanzisha uchunguzi kuhusu tuhuma kuwa mkuu wa shirika la habari la taifa la SABC, amepewa mwanamke kama zawadi.Tume ya usawa wa kijinsia imesema imepokea malalamiko baada ya taarifa kuwa mkuu huyo Hlaudi Motsoeneng alipewa mke na machifu wa kijadi.
Machifu hao walikuwa sehemu ya kundi la watu wa jadi waliokuwa wakiomba matangazo yaongezwe katika lugha ya Venda.Serikali imesema tabia hiyo "inasikitisha".Tukio hilo inasemekana limetokea wakati wa ziara ya mkuu huyo katika jimbo la Limpopo.

Wanawake kumi walipita mbele ya mkuu huyo, na akamchagua anayemtaka. Taarifa zinasema wazazi wa wasichana hao walikuwepo na walikuwa wakifahamu kinachotokea na walikubali.

No comments:

Post a Comment