Social Icons

Saturday 21 June 2014

Habari Kuhusu Kuuwawa Kwa Mwandishi wa Habari Huko Mogadishu Kwenye Mlipuko wa Bomu


Mwandishi wa habari kijana wa Somalia ameuwawa kwenye mripuko wa bomu lilotegwa chini ya gari lake mjini Mogadishu.Yusuf Keynan alikufa wakati bomu hilo liliporipuka alipotia moto gari, akitaka kuelekea kazini.


Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu anasema Yusuf Keynan (aliyefanya kazi katika redio Mustaqbal), alikuwa mwandishi wa habari kijana aliyekuwa akipendwa na hodari katika kazi yake.

Huyo ni mwandishi wa habari wa kwanza kuuwawa nchini Somalia mwaka huu, baada ya waandishi habari kadha kuuwawa kwa mfululizo katika miaka miwili iliyopita.Shirika la Kuwalinda Waandishi wa Habari linasema kuwa Somalia ni moja kati ya nchi hatari kabisa kwa waandishi.Hakuna aliyedai kuhusika na mauaji ya kijana huyo.

Source; BBC swahili

No comments:

Post a Comment